Sibuka FM

Dc Maswa awashukia viongozi wazembe

23 April 2024, 6:12 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akizungumza na wananchi katika kijiji cha Lalago Picha na Paul Yohana

Wananchi wakeleka na utendaji kazi wa wenyeviti wa vitongoji na vijiji kushindwa kuwasikiliza kero zinawakabili ambazo zipo kwenye uwezo wa viongozi hao hivyo kuondoa uaminifu kwao

Na,Paul Yohana

Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge awewataka wenyeviti wa vitongoji na vijiji kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi ili kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi na siyo kusubiri viongozi wa ngazi za juu.

Aswege Kaminyoge ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Simiyu uliofanyika katika kijiji na kata ya Lalago ambapo amesema kuwa wenyeviti wa vitongoji na vijiji wahakikishe  wanafanya mikutano ya hadhara ambayo ipo kisheria ili kusikiliza kero zinazowakabili wananchi na kuona namna nzuri ya kuzitatua.

Sauti ya Dc Maswa akitoa maagizo kwa viongozi kufanya mikutano ya hadhara.

Kaminyoge amesema kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi billion 10 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya,elimu na miundombinu ya barabara.

Sauti ya Dc Maswa akielezea mafanikio ya miradi ya maendeleo

Kaminyoge ameongeza kuwa katika swala la umeme wilaya ya Maswa imepiga hatua kubwa kwani mpaka sasa umeme umepelekwa katika vijiji vyote 120 hivyo katika bajeti ya mwaka wa fedha  2024/2025  watapeleka umeme kwenye vitongoji hivyo wananchi wawe na subira.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza mkutanoni hapo

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Simiyu,Shamsa Mohamed ametoa wito kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya chini hadi juu kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kutokana na fedha zinazoletwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili iweze kuleta thamani ya fedha zilizotumika na kuweza kumunufaisha wananchi moja kwa moja.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM mkoa Bi.Shamsa Mohamed akitoa wito kwa viongozi