Sibuka FM

DC Maswa akabidhi pikipiki kwa  CBWSOs

7 May 2024, 7:54 pm

Afisa Maendeleo ya Jamii wa RUWASA Willison Magaigwa (mwenye shati nyeupe mbele ) akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge wakati wa Hafla ya kukabidhi Pikipiki kwa CBWSOs kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa Shughuli katika Jumuiya hizo. Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge amewataka viongozi wa CBWSOs zilizogawiwa pikipiki kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa ili kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za maji na siyo shughuli binafsi zisizo na tija.

Na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa, mkoani Simiyu  Mhe, Aswege  Kaminyoge  amekabidhi pikipiki nne aina  ya  TVS   zenye  thamani ya  shiilingi milioni kumi  na  sita kwa ajili  ya  kurahisisha shughuli  za Jumuiya  ya   Watoa  huduma  ya  Maji  ngazi  ya  Jamii  (CBWSOs)  kupitia  Wakala wa  Maji  na  Usafi wa  Mazingira  Vijijini – RUWASA   Wilayani  Maswa

Akikabidhi  pikipiki   kwa  Viongozi  wa  Jumuiya  za  Watoa  Huduma  za  Maji, Mkuu  huyo  wa  Wilaya  amesema  kuwa   lengo  la  pikipiki  hizo ni   kwenda  kusaidia  Jamii  husika katika  kutatua  changamoto  kwenye  Utoaji  wa huduma za Maji  na  siyo kuzifanyia  Shughuli  binafsi

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Kaminyoge

Mhe,  Kaminyoge  ameongeza  kuwa    Mhe  Rais  Samia  ametoa  fedha  nyingi  katika  Wilaya  ya  Maswa  ambapo  Miradi  Mikubwa   ya Maji  kila   vijiji  na kata   inaendelea  kutekelezwa    na  kutoa  Wito  kwa  Meneja  RUWASA   Wilayani  hapa  kuwasimamia  kikamilifu  Wakandarasi  Wakamilishe  kwa  Wakati  ili kupunguza  Adha ya Maji

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Kaminyoge
Mkuu wa Wilaya ya Maswa akiendesha pikipiki mojawapo alizokabidhi kwa CBWSOs

Mhandisi  Lucas  Madaha  ni  Meneja   Ruwasa  Wilayani  Maswa   amesema  kuwa   Wamejikita   kuziwezesha   CBWSOs   katika  Utekelezaji  wa  Majukumu  yake  kwa  Wananchi  na  kuongeza  Upatikanaji  wa  Huduma  za  Maji  Vijijini

Sauti ya Mhandisi Lucas Madaha Meneja wa RUWASA Wilaya ya Maswa

Akitoa   Taarifa  ya  Utekelezaji  wa  Miradi ya Maji  na  Ununuzi  wa  Pikipiki  Afisa  Maendeleo ya Jamii wa  RUWASA  Wilayani hapa   ndugu  Willison  Magaigwa  amesema  kuwa  kwa  Sasa  upatikanaji  wa  Maji  umeongezeka kutoka  Asilimia 68.9%  hadi  kufikia  Asilimia  74.6% kwa  Sasa  huku  akitaja  changamoto  zinazowakabili  Jumuiya za Watoa  Huduma  za  Maji

Sauti ya Willison Magaigwa -Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Maswa

Kwa  Upande  wake  Mkandarasi   anayetekeleza  Miradi  ya  Maji  Wilaya  hapa  amesema  kuwa  anamshukuru  Rais  Samia  kwa  kutoa  tenda  kwa  Kampuni za  Wazawa hivyo kuahidi kukamilisha  kwa  Wakati  ili Wananchi  Wanufaike  na  Miradi  hiyo

Sauti ya Sami Lema Mkandarasi anayetekeleza Miradi ya Maji Maswa

 Steven  Fabiani  Biseko  ni  miongoni  mwa  Viongozi  wa CBWSOs  waliokabidhiwa  Pikipiki  amesema  kuwa   Watazitunza   na  kuzitumia  kwa  Manufaa ya  Taasisi  na   siyo  binafsi ili  zilete  Mabadiliko  katika  utoaji  wa  Huduma  za  Maji  Vijijini

Sauti ya Steven Biseko Mnufaika wa Pikipiki