Sibuka FM

Wazazi wa kidigitali ni chanzo cha ukatili kwa watoto Maswa

6 May 2024, 11:22 am

Pichani ni mkuu wa dawati la kijinsia jeshi la polisi wilaya ya Maswa,Afande Magreth Mwinuka Picha na Alex Sayi

Kushiriki kikamilifu kwa wazazi na walezi kumetajwa kumaliza ukatili kwa watoto ambao wanafanyiwa ukatili katika jamii zao hasa mtoto kuanzia kipindi cha ujauzito hadi kufikia umri wa miaka (8).

Na Alex.F.Sayi

Imebainishwa kuwa wazazi na walezi wamekuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa watoto kufuatia tabia ya wazazi wa sasa kutokuwa na muda wa kutosha wakufanya  uangalizi kwa watoto.

Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ,Magreth Mwinuka ambae ni mkuu wa dawati la jinsia wilayani hapo ambapo amesema kuwa mara nyingi wazazi na walezi ambao wanafanya kazi za umma au binafsi wamekuwa hawana muda wa kukaa na watoto wao hivyo mfanyakazi wa ndani ndiye amekuwa kama mzazi.

Sauti ya mkuu wa dawati la kijinsia wilaya ya Maswa wa jeshi la polisi,Magreth Mwinuka

Mwinuka amesema kuwa kunahaja ya wazazi na walezi kutenga muda wakuwalea watoto na kutokuwaacha watoto kujisimamia wenyewe.

Sauti ya Magreth Mwinuka

Awali akizungumza na Sibuka fm amesema kuwa kwa asilimia kubwa wazazi wanapelekea ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa kujua au kwa kutokujua.

Sauti ya afande Magreth Mwinuka

Akizungumza kwa njia ya simu Masunga Eliasi amelishukuru jeshi la polisi kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya malezi kwa watoto hali ambayo itasaidia kujirudi kwa wazazi wenye tabia kama hizo.

Sauti ya Masunga Elias akilishukuru jeshi la polisi