Msimu wa ununuzi wa pamba 2024/2025 Wazinduliwa rasmi Maswa
15 May 2024, 8:57 pm
Mkuu wa Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mazao amezindua msimu wa ununuzi wa pamba 2024/2025 Wilayani hapa na kuzitaka kampuni zote zinayodaiwa ushuru wa musimu uliopita hazitaruhusiwa kuanza kununua kabla ya kulipa madeni yao.
Msimu wa Ununuzi wa zao la pamba ( dhahabu nyeupe) 2024/ 2025 wilayani Maswa umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya Mhe Aswege Kaminyoge na kuwataka wanunuzi wa zao hilo kuweka utaratibu mzuri usiokuwa na maswali na manung’uniko kwa pande zote.
Mh Kaminyoge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazao Wilayani hapa amesema kuwa kabla hawajaanza kununua rasmi Wakae kwa Pamoja na Wadau wengine wa Pamba ili kuweka sawa namna ya ulipaji wa Fedha kutoka kwa Kampuni za Ununuzi kwenda kwa Amcos na kutoka kwa Amcos kwenda kwa Wakulima
Mwakilishi wa Bodi ya Pamba Wilayani Maswa Ally Mabrouk ametoa utaratibu wa kampuni ipi itanunua maeneo gani na Kuwataka kufuata Utaratibu uliowekwa na Bodi ya Pamba na Kampuni itakayokiuka Mashariti ya Ununuzi , Pamba yake itataifishwa na Serikali pamoja na Kufutiwa Leseni
Maisha Mtipa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ameshauri kampuni za Ununuzi kuangalia Usalama wa Fedha zao wanazowekeza kwenye Amcos ili wanunuliwa Pamba na siyo kukimbilia kununua tu bila kuweka Makubaliano Mazuri kati ya Kampuni ya Ununuzi na Amcos
Kwa Upande wake Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Simiyu Ndugu Falesi Muganda ametoa rai kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (Amcos ) wanapaswa kuwa Wazalendo na Waadilifu kwani wanajukumu kubwa la Kuwasaidia Wakuima na siyo kuwaibia.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kilimo cha Pamba , Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Robert Urasa amesema kuwa Malengo ya Uzalishaji yameshindwa kufikiwa kutokana na Mvua zilizonyesha juu ya Wastani zilipelekea baadhi ya kulima Kushindwa kulima Zao hilo
Naye Meneja Wakala wa vipimo Mkoa wa Simiyu Francis Olwero amewataka Viongozi wa Amcos kupeleka Mizao yote kwenda kuhakikiwa na kuwekewa Mhuri kwa ajili ya kutumika katika Ununuzi wa Zao la Pamba na Wasikubali kutumia Mizani ambayo haijahakikiwa na Wakala wa Vipimo kwani watakuwa wanaingia kwenye Mgogoro na Serikali