Sibuka FM

RUWASA Simiyu yatakiwa kulipa wakandarasi kwa wakati

26 April 2024, 10:30 am

Pichani ni naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Simiyu akitoa taarifa ya utekelezaji kwa waandishi wa habari Picha na Daniel Manyanga

Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) mkoani Simiyu kuwalipa wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali kwa wakati ili kuondokana na kuisababishia serikali hasara itokanayo na ucheleweshaji wa malipo.

Na,Daniel Manyanga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu wameishauri wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA)mkoani hapo kuwalipa wakandarasi  malipo wanayodai kwa wakati kiasi cha zaidi ya Tsh billion 6.1 ili kuepuka kuisababishia serikali hasara itokanayo wa ucheleweshaji wa malipo.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa (TAKUKURU)mkoa wa Simiyu ,Aron Misanga wakati  akitoa taarifa  ya utekelezaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 kwa waandishi wa habari ofisini kwake.

Misanga amesema kuwa uchelewashaji wa fedha hizo unaweza kuisababishia hasara serikali ikiwa wakandarasi hao wataomba riba itokanayo na ucheleweshaji wa malipo yao.

Sauti ya naibu mkuu wa TAKUKURU akizungumza na waandishi wa habari

Misanga ameongeza kuwa TAKUKURU katika kipindi hicho ilipokea jumla ya taarifa 44 kati hizo 33 zilihusu rushwa na 11 hazikuhusiana na rushwa.

Sauti ya naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Simiyu

Katika hatua nyingine Aron Misanga amebainisha kuwa chunguzi (10)zimekamilika na majalada kuwasilishwa ofisi ya taifa ya mashitaka na mashauri mapya (10) yamefunguliwa mahakamani nakufanya mashauri (15)kuendelea mahakamani ambapo kati ya hayo mashauri(08) yaliamuliwa na upande wa jamhuri kushinda  mashauri yote(08).

Sauti ya Aron Misanga akifafanua ushindi wa jamhuri katika mashauri