Sibuka FM

March 31, 2021, 4:48 pm

Jeshi la polisi mkoani Simiyu linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kupatikana na nyara za serikali.

RPC Simiyu ACP Richard Abwao

Haya yamesemwa   na kamanda wa jeshi hilo mkoani hapo ACP Richard Abwao wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari na kuongeza kuwa mtuhumiwa alikutwa akiwa na mabegi matatu yakiwa na  kobe 438 wenye thamani ya shilingi  milioni 71.1.

“mnamo marchi 21 ,2021 majira ya saa mbili usiku huko katika maeneo ya

Aidha ameongeza kuwa mtuhumiwa yupo mahabusu na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi mkoani hapo kuepuka makosa ya jinai kwa  kujiepusha na umiliki wa nyara za serikali kinyume na sheria  huku akiwataka kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu.

sauti ya RPC Simiyu