Sibuka FM

Kanisa kushiriki ujenzi wa makaravati Maswa

13 December 2023, 1:37 pm

Pichani:Kulia ni Bishop Adam Gige mwenye Suti nyeusi aliye katikati ni muumini,kushoto ni Mama Bishop Bi,Eliwaja Adam Gige wakitoa msaada wa chakula kwa muumini. Picha na Alex Sayi

Zaidi ya  Sh.Mil,15 kutumika kufanya Ujenzi wa Karavati(3)kwenye baadhi ya mitaa  Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.

Na Alex Sayi

Kanisa la Repentence Pentacost Mission Church of Tanzania (RPMT) limekabidhi karavati moja lenye gharama ya  zaidi ya Sh.Mil 5 kati ya madaraja matatu yanayotarajiwa kujengwa na Kanisa hilo.

Hayo yamesemwa na Askofu wa Kanisa hilo Bishop Adam Gige kwenye hafra yakuadhimisha miaka (12) ya Kanisa hilo iliyofanyika kwenye viwanja kwa Kanisa hilo Desemba 10 Mwaka huu.

Pichani:Bishop Adam Gige.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Bishop Adam Gige

Akisoma lisala mbele ya mgeni rasmi Elibariki Adam Gige amesema kuwa Kanisa limefanikiwa pamoja na mambo mengine kufanya Ujenzi wa Kanisa,Tank la Maji, kutoa msaada wa Nguo,Chakula (Mchele na Mahindi) vyote vikiwa na gharama ya Sh.Mil 3.2.

Pichani:Elibariki Adam Gige.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Elibariki Adam Gige

Kwa upande wake kaimu Mwenyekiti Kitongoji cha Standi Mpya Kata ya Shanwa Wilayani hapa Julius Kabelele alilishukuru Kanisa hilo kwa msaada huo huku akiomba wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo

Sauti ya Kaimu Mwenyekiti Kitongoji Julius Kabelele

Aidha mgeni rasmi kwenye halfa hiyo Afisa Tarafa,Tarafa ya Sengerema Saguda Sayayi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa amesema kuwa Serikali inatambua mchango uliofanywa na Kanisa hilo

Pichani:Mgeni rasmi Saguda Sayayi
Sauti ya Saguda Sayayi Afisa Tarafa Sengerema
Pichani:Kulia ni Bishop Pius Masinde toka Kenya,katikati,Bishop, Julius Towet toka Kenya wa tatu Bishop Saimon Betty toka Kenya wa nne ni Apostle Deni Okid toka Uganda wakiwa ni wageni waalikwa kwenye hafra ya kuadhimisha miaka (12)ya Kanisa la (RPMT)BEROYA MASWA.Picha na Alex Sayi.