Sibuka FM

DC Simalenga atangaza usafi wa mji, ataka kuundwa vikundi

19 August 2026, 06:08

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kikao. Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Tunahitaji kuuweka mji wetu katika mazingira ya usafi ili kulinda heshima tuliyopewa ya mji hivyo kila mtumishi wa umma na wananchi kwa ujumla tunao wajibu wa kuufanya mji wetu kuwa safi majira yote na hii itasaidia sana katika mapambano ya magonjwa ya milipuko”. 

Na,Daniel Manyanga

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga ameitaka halmashauri ya mji wa Bariadi kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha wakazi wa mji huo hawafanyi uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mji huo ili kulinda hadhi ya mji huo na kuepuka mlipuko wa magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Simalenga ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambapo amesema kuwa ni muhimu usafi wa mazingira uzingatiwe na kuagiza kuundwa vikundi vya usafi katika barabara za mji huo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga

Nashon Ngussa wa kata ya Isanga, Nkamba Zabron diwani wa kata ya Bunamhala na Martine Singibala  diwani wa kata ya Mhango katika halmashauri hiyo wameiomba TARURA wilayani Bariadi kuzifanyia matengenezo barabara zilizoharibika katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha mawasiliano ya barabara kwa watumiaji wa miundombinu hiyo ikiwa pamoja na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

Sauti ya madiwani wakiomba matengenezo ya barabara korofi

Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) wilaya ya Bariadi,Mhandisi Hussein Katakwebah, ameitaja bajeti ya TARURA kwa mwaka wa fedha 2026/2027 na kwamba wameanza kutangaza kazi za matengenezo ya barabara.

Sauti ya meneja wa TARURA wilaya ya Bariadi, Mhandisi Hussein Katakwebah