Sibuka FM

CCWT, benki kuingia makubaliano ya kukopesha wakulima, wafugaji

8 October 2023, 9:24 am

Mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza kwenye Kongamano la Vijana lililofanyika ukumbi wa halmashauri wilayani Maswa lililoandaliwa na kikundi cha vijana cha AGRIWWEN.Picha Na Alex Sayi.

Vijana wasomi nchini wametakiwa kubadili fikra za kuendelea kusubiri kuajiriwa serikalini na badala yake wachangamkie fursa za ajira  zaidi ya 500,000 zilizopo kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.

Na Alex Sayi

Chama Cha Wafugaji Tanzania CCWT kimebainisha kuwa kinaendelea na mchakato wa kukubaliana na benki nchini ili wafugaji na wakulima waweze kukopesheka.

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Kusundwa  Wamalwa wakati akizungumza na vijana kwenye kongamano la vijana  lililolenga kubainisha fursa za uchumi kwa vijana lililofanyika Oktoba 6, 2023 ukumbi wa halmashauri ya wilaya Maswa.

Wamalwa amesema kuwa bado wanaendelea na makubaliao na sekta hiyo za benki ili wafugaji na wakulima waweze kukopesheka kwa mikopo ya riba nafuu na ya muda mrefu.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti (CCWT)Kusundwa Wamalwa

Sanjari na hilo Wamalwa ameongeza kuwa jamii ya kifugaji inapaswa kubadilika na kujenga tabia ya kuhudhuria kwenye mikutano ya hadhara ambako sheria ndogondogo huundwa ili wafugaji wawe sehemu ya uandaaji wa sheria hizo.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti (CCWT)Kusundwa Wamalwa
Makamu Mwenyekiti wa CCWT Kusundwa Wamalwa akizungumza wakati wa kongamano la vijana. Picha Na,Alex Sayi.

Akizungumza kwenye kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya hiyo Aswege Kaminyoge  amesema kuwa Rais Samia Suluhu  tayari alishaziwezesha benki nchini ili ziweze kuwakopesha vijana, wakulima na wafugaji, hivyo kuwataka  vijana wachangamkie fursa hizo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Maswa Aswege Kaminyoge.

Philibet  Akili mfugaji na mkulima wilayani hapa amekiomba chama cha wafugaji taifa kuwapamabania  zaidi wafugaji na wakulima kuhakikisha kuwa wanakopesheka huku akiomba ofisi ya kilimo kupunguza urasimu wa  upatikanaji wa mbengu za majani ya malisho.

Sauti ya Philibet Akili

Akisoma risala kwa mkuu wa wilaya Bw. Peter Paschal ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha vijana  cha AGRIWEEN, waandaaji wa kongamano hilo amewataka vijana kuchangamkia fursa kwenye sekta ya kilimo na ufugaji kwa kuwa sekta hiyo inatoa  fursa ya ajira zaidi ya 500,000.

Aidha Paschal ameongeza kuwa kuna kila sababu ya vijana kuondokana na fikra za kusubiria kuajiriwa na serikali kwa kuwa kwa sasa  soko la ajira serikalini ni finyu ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka.

“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 toka Ofisi Kuu ya Takwimu Taifa inaonesha kuwa  idadi ya vijana wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka ni kati 800,000 hadi 1,000,000 wanaopigania nafasi za ajira  zisizozidi 60,000 katika sekta ya umma, huku kukiwa na nafasi takribani 300,000 sekta binafsi hivyo kulazimika kuacha vijana kati ya 400,000 hadi 600,000 wakiwa hawana ajira kila mwaka.” Alisema Paschal.

Wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha AGRIWEEN, wa pili ni Makamu Mwenyekiti(CCWT)Kusundwa Wamalwa, wa tatu kulia ni Mathayo Daniel Katibu(CCWT).Picha na Alex Sayi.