Sibuka FM

Maswa: Wazazi waaswa kuwasomesha watoto elimu ya ufundi

28 November 2023, 2:55 pm

Pichani:Kushoto wa (4)Mkuu wa Chuo Malampaka Michael Mahundi,wapili ni (Mb) wa Maswa Magharibi Mashimba Ndaki,wa tatu kulia Diwani wa Kata hiyo Renatus Mashala,mwenye hijabu Bi,Mgeni Umba Mtendaji Kata Kijiji Malampaka,wakwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo Malya Frank Igembe.Picha na Alex Sayi

Wazazi waaswa kuwasomesha Watoto wao Elimu ya Ufundi ili kukabiliana na obwe la ukosefu wa ajira uliopo Serikalini kwa hivi sasa.

Na,Alex Sayi.

Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki amewaasa wazazi/walezi kuwasomesha watoto wao Elimu ya Ufundi ili kukabiliana na soko la Ajira.

Hayo  yamesemwa na (Mb)huyo wakati akiwahutubia wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi  Malampaka kilichopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu kwenye mahafali ya (47)ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 24,mwaka huu kwenye Ukumbi wa Chuo hicho.

Sauti ya (Mb)wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki

Mashimba ameongeza kuwa kuna haja ya Watoto kuwasomesha Elimu ya Ufundi ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiria ajira Serikalini ,huku akiahidi kuwapatia mtaji wahitimu wa Chuo hicho

Sauti ya (Mb)Mashimba Ndaki
Pichani:Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki akimtunuku cheti mhitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka.Picha na Alex Sayi

Diwani wa Kata hiyo Renatus Mashara amesema kuwa maisha ya sasa yanahitaji kuwa na Elimu na  Elimu inayohitajika  ni  Elimu yakujitegemea,hivyo kutoa wito kwa wazazi kuwasomesha Watoto wao.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Malampaka Renatus Mashara

Mjumbe wa Bodi wa Chuo hicho Charles Buluge amewaomba wazazi na walezi  wazawa wanaokizunguka Chuo hicho waone umuhimu wa kuwasomesha Watoto wao ili wapate Elimu itakayowasaidia kulima na Kufuga kisasa.

Mhitimu wa Chuo hicho na Rais wa Chuo hicho Charles Joseph amesema kuwa Elimu waliyoipata inawasaidia kujitegemea na kutokuwa tegemezi kwa Serikali na kwa wazazi.

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka Michael Mahundi amesema kuwa anaishukuru Serikali ya awamu ya (6)kwa kukikumbuka Chuo hicho nakukitengea  fedha za uboreshaji wa  Chuo hicho.

Pichani:Anaezungumza ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka Wilayani Maswa Mkoani Simiyu:Picha na Alex Sayi