Jamii ya wafugaji, wadzabe wanufaika na mafunzo ya sheria ya ardhi
4 April 2024, 5:31 pm
Jamii ya wafugaji na Wahadzabe wamenufaika na mafunzo ya Sheria ya Ardhi kwa lengo la kuzisaidia jamii hizo kujua hatua za utatuzi wa migogoro kwenye maeneo yao.
Na,Alex Sayi
Shirika la DANMISSION kwa ushirikiano na kanisa la KKKT Jimbo la Bariadi Mjini Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wameziwezesha jamii za kifugaji na jamii za waokota matunda na wawindaji asilia(Hadzabe)kupata uelewa wa Sheria ya Ardhi ya mwaka (1999)
Hayo yamesemwa na mwanasheria kutoka Shirika la Pastoralists Indigenous Non-Governmental Organazation’sForum(PINGO’S FORUM)Saitoti Parmelo wakati wa wafunzo yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Sunga Kingdom Hotel Mkoani Simiyu.
Parmelo ameongeza kuwa lengo la mradi huo nikuzileta pamoja jamii za wafugaji ,wawindaji na waokota matunda asilia ili kujadili changamoto zinazozikabili jamii hizo.
Kwa upande wake Afisa Mipango,Miradi na Afya toka Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Martha Mwakisu amesema kuwa mradi umelenga kuziwezesha jamii hizi kuwa na uwezo wakujitegemea kwenye utatuzi wa migogoro pale inapojitokeza.
Samson Salehe mshiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa jamii ya Wahadzabe wamefurahi kupata fursa hiyo yakupata mafunzo hayo kwakuwa ni jamii ambayo inakabiliwa na changamoto yakupoteza asili yake.