Sibuka FM

Kamati ya bunge yaridhishwa mradi hatimiliki Maswa

13 November 2023, 4:58 pm

Pichani:Kulia ni Naib Waziri wa Ardhi,Nyumba Maendeleo na Makazi Geophrey Pinda akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi,Maliasili na Utalii Timothy Mzava,kushoto ni Bi, Najima Giga (Mb) Viti maalum toka Mkoa wa Mjini Zanzibar.Picha na Alex Sayi.

Mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi vijijini unaotekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu unatarajia kutoa hatimiliki 100,000 kwa wananchi.

Na Alex Sayi

Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhika na utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi vijijini unaotekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Timothy Mzava (Mb) jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga  wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwadila kata ya Sukuma eilayani hapa kwenye mkutano wa hadhara.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Timothy Mzava

Mzava ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo utasaidia  kuondoa migogoro kati ya kijiji na kijiji, shamba na shamba, kiwanja na kiwanja na kuongeza thamani ya ardhi na kuwasaidia wananchi kuboresha maisha yao.

Sauti ya Mwenyekiti Mzava
Pichani:Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi,Maliasili na Utalii Timothy Mzava.Picha na Alex Sayi.

 Geophrey Mizengo Pinda Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba Maendeleo na Makazi amesema kuwa wilaya ya Maswa ni miongoni mwa wilaya 7 za awali zinazonufaika na utekelezaji wa mradi huo ikiwemo Mufindi, Songwe, Mbinga, Chamwino, Longido na Tanganyika.

Sauti ya Naib Waziri Ardhi,Nyumba Maendeleo na Makazi Geophrey Pinda

Vivian Christian amesema kuwa mradi unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano 2022-2027  kwa  wilaya ya Maswa na mradi ulianza Feb, 2023 hadi kufikia Novemba 10/2023 mradi umetumia Sh.Mil 819.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Maswa Vivian Christian

Ibrahim Jagadi mkazi wa Mwadila akizungumza na Sibuka Fm amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwapatia hatimiliki bure kwa kuwa awali upatikanaji wa hati hizo ilikuwa ni gharama kubwa na usumbufu ulikuwa ni mkubwa mno.

Sauti ya Ibrahim Jagadi

Sahani  Dwese  akizungumza na Sibuka Fm amesema kuwa upimaji wa maeneo unasaidia kuondoa migogoro kwenye makazi na mipaka ya mashamba kwa kuwa kila mtu anakuwa anajua eneo lake linaishia wapi.

Sauti ya Sahani Dwese.
Pichani:Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mwadila Kata ya Sukuma Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wakisikiliza kwa makini kwenye mkutana wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.Picha na Alex Sayi.