Sibuka FM

Madiwani Maswa wakerwa na majibu ya TARURA

19 November 2023, 4:37 pm

Pichani:Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Maswa Paulo Maige,Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Maswa Vivian Christian,wa tatu kilia Katibu (CCM)wilaya John Mapanga,na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri Ndila Mayeka wa tatu Mwisho ni (Mb) wa Maswa Magharibi Mashimba Ndaki.Picha na Alex Sayi.

 TARURA wilayani Maswa mkoani Simiyu inayohudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya Km 184.2 na iliyofikia 77% ya Barabara zinazopitika kwa nyakati zote za msimu sawa na km 837.39 imelalamikiwa kwakushindwa kupeleka   kwa wakati wakandarasi kwenye baadhi ya Barabara Wilayani hapa.

Na Alex Sayi

Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Wilayani Maswa Mkoani Simiyu umelalamikiwa na baadhi ya Madiwani kwa kushindwa kupeleka wakandarasi kwenye baadhi ya Barabara korofi kwa zaidi ya miaka (10) sasa.

Hayo yamesemwa na baadhi ya Madiwani hao kwenye Baraza la Madiwani lililoketi Nov 17 Mwaka huu kwenye ukumbi wa Halmashauri, huku baadhi ya Madiwani hao wakionekana kusikitishwa na majibu ya ubabaishaji yaliyokuwa yakitolewa na Mwakilishi wa Meneja (TARURA) Wilayani hapa.

Perus Makalwe Diwani wa Viti maalumu amesema kuwa licha ya taarifa kufika Ofisi za (TARURA)kwa zaidi ya miaka (10)kuhusiana na Barabara ya Mwakaleka,Bugalama,Bugolola bado (TARURA)wameshindwa kufanyia kazi suala hilo.

Pichani:Diwani wa Viti Maalumu Perus Makalwe,Picha na Alex Sayi
Sauti ya Perus Makalwe Diwani Viti Maalumu

Stiven Dwese Diwani wa Kata ya G’wigwa Wilayani hapa amesema kuwa baadhi ya Barabara zilizochongwa na kuwekewa molamu zimeanza kukatika kutokana na Mvua chache zinazonyesha hivyo kuwaomba (TARURA) kuimarisha ubora wa Barabara hizo

Pichani:aliyesimama ni Diwani wa Kata ya Ng’wingwa Steven Dwese,aliyekaa kushoto Mh,Emmanuel Dogani.Picha na Alex Sayi.
Sauti ya Stiven Dwese Diwani Kata ya Ng’wingwa

Sadick Duttu Diwani wa Kata ya Senani Wilayani Maswa Mkoani hapa alitaka kujua nini kinasababisha wakandarasi  kushindwa kufika site  kwa wakati licha ya fedha kutengwa kwa muda mrefu

Sauti ya Sadick Duttu Diwani Kata ya Senani

Paulo Maige Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Wilayani hapa alisema kuwa itapendeza ikiwa (TARURA)watakuwa na majibu yauhakika na sio kutoa majibu ya kubabaisha mbele ya Baraza hilo,Maige alisema hayo baada ya msemaji wa (TARURA) kushindwa kuwa na majibu sahihi kwa swali lilioulizwa na Diwani wa Kata ya G’wingwa Stiven Dwese kuhusiana na Barabara ya  Sola,Sakasaka Mwandoya.

Sauti ya Poulo Maige Diwani Kata ya Shanwa na Mwenyekiti Halmashauri Maswa na Edward Jinai Mwakilishi wa Meneja Tarura Maswa.