Sibuka FM

DC KAMINYOGE ;  Wananchi  Jitokezeni   kwenye  Mikutano  ya  Hadhara

3 April 2024, 10:20 am

Pichani aliyesimama mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Bugalama katika Kampeni yake ya Kusikiliza Kero za Wananchi katika Wilaya yake. Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mkoani  Simiyu  Mhe,  Aswege  Enock  Kaminyoge  amewataka  Wananchi  wilaya  hapo  kujitokeza  kwa  Wingi  katika  Mikutano  ya   Hadhara  inayoitishwa  na  Viongozi  wao  wa  Vijiji  na  kata  ili  kutoa  kero  zao  na  changamoto  mbalimbali  zinazowakabiri.

Mh  Kaminyoge  amesema  Mikutano  ya  Hadhara   ndio  sehemu  sahihi  ya  kupata  taarifa  za  maendeleo  ya  vijiji   na   utatuzi  wa  changamoto  zake  lakini  pia   ni  Utekelezaji  wa  Dhana  ya  Utawala  Bora

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na Wananchi wa Bugalama

Aidha  Mh Kaminyoge  amezitaka  Taasisi  zote   za  Serikali   kuhakikisha  wanapima  na Kutambua  mipaka  ya  maeneo  yote   ili  kuepuka  Migogoro  ya   Mipaka  dhidi  ya  Wananchi  hivyo  maeneo  yote  yaliyovamiwa  na  Wananchi  yarudishwe  mara  moja

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akizungumza na Wananchi wa Bugalama

Akitolea  Ufafanuzi  malalamika  yaliyo yaliyotolewa   na  Wananchi  juu  ya  Utaratibu  wa  Matibabu   ya  Bima  ya  Afya  iliyoboreshwa  CHF  Muuguzi  Mfawidhi  wa  Zahanati  ya   Bugalama  Tumpe  Mkussa   amesema   Utaratibu  wa  CHF    mwanacha  anapaswa  kutibiwa  mara tatu  hadi  mara  Nne  kwa  Mwezi

Sauti ya Tumpe Mkussa Muuguzi Mfawidhi Zahanati ya Bugalama akifafanua kuhusu CHF

Ngude  Balunhya  ni  Mwenyekiti  wa  Serikali  ya  Kijiji  cha  Bugalama , kata  ya  Bugalama  Wilayani  Maswa  amesema  wananchi  wengi  hawahudhurii  Mikutano  ya  Hadhara hivyo  baadhi  yao  kuuliza  Maswali  yaliyofanyiwa  Utatuzi  likiwepo  suala  la   Wafugaji  kutozwa  fedha  kubwa  ya  Kuoshea  Mifugo  yao.

Sauti ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bugalama Ngude Balunhya

Awali   baadhi  ya  Wananchi  wa  Bugalama  walipaza  sauti  zao za  Kero  kwa  Mkuu  wa   Mkuu  wa  Wilaya   ya  Maswa  na  Kumuelezea  Kero  ya  Watendaji  wanaokula  Fedha  za  Wananchi  kisha kuhamishiwa  kwenye Vituo  vingine  bila   Kuchukuliwa  hatua zozote huku Mkuu wa Wilaya akitoa maelekezo kwa Mtendaji aliyehamishwa Kurudi kweney Kijiji hicho

Sauti ya Mwananchi Bugalama na Mkuu wa Wilaya Maswa

Wananchi wa Kijiji cha Bugalama Wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mh Aswege Kaminyoge ambaye hayupo Pichani.