Sibuka FM

DC Simalenga ataka kukamilika kwa sekondari kabla ya januar 2027

27 July 2026, 13:47

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akiwa kwenye moja wapo ya shughuli za serikali mkoani hapo Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

“Kila mtu anahaki ya kupata huduma bora bila kujali itikadi zao ili kufikia malengo yake tumetengeneza miundombinu bora nchini kwa kila sekta”.

Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Simon Simalenga amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi kuanza mara moja ujenzi wa shule mpya ya sekondari Matongo, iliyopo  kata ya Matongo wilayani hapo na kuhakikisha  ifikapo mwezi Januari 2027 wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo.

Simalenga ametoa agizo hilo baada ya kufika katika kata hiyo na kukagua zoezi la uchimbaji wa msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hiyo ambapo amesema ni muhimu ujenzi huo ukaanza kwa haraka kwa ajili ya kuwaondolea wanafunzi wa kata hiyo changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo ya sekondari.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa,Simon Simalenga

Khalid Mbwana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi, amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wa vijiji vya Matongo na Salalia kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu pamoja na vishawishi  hasa kwa wanafunzi wa kike.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi

Samson Katambi, Kimola Sayi na Masunga Keya ni baadhi ya wakazi wa kata ya Matongo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo na kusema kuwa itaondoa changamoto ya wanafunzi kukatisha masomo yao kutokana na umbali wa shule.

Sauti ya wananchi