Sibuka FM

Chanjo ya polio kutolewa nyumba kwa nyumba Maswa

5 May 2026, 00:16

Mhe Anna Gidary kaimu DC Maswa, kulia kwake ni Ndugu Athumani Kalaghe katibu tawala wilaya ya Maswa na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Maswa ndugu Maisha Mtipa wakiwa katika kikao cha uhamasishaji wa zoezi la chanjo ya Polio linalofanyika tarehe Mei 7-10, 2026. PICHA na Nicholaus Machunda

Zoezi hili ili lifanikiwe liwashirikishe hadi viongozi wa ngazi za chini kama vile wenyeviti wa vijiji na Vitongoji na mabalozi ili kuondoa upotoshaji unaojitokeza ” Mhe Anna Gidarya -Kaimu DC Maswa “

Zoezi la  Utoaji wa Chanjo ya  Polio  awamu ya pili Wilayni  Maswa, Mkoani  Simiyu itatolewa  kuanzia tarehe 7 hadi 10 mwezi huu wa  tano ambapo mkakati  wa serikali ni kupita nyumba kwa nyumba ili  kuhakikisha watoto wote wanafikiwa  na  zoezi  hilo

Hayo yamesemwa  na Afisa  Afya Mkoa  wa  Simiyu  Bashiri  Salum  wakati  wa kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali  chenye lengo  la uhamasishaji wa chanjo  hiyo  kilichofanyika katika  ukumbi  wa  ofisi ya mkuu wa Wilaya.

Sauti ya Bashiri Salum afisa afya Mkoa wa simiyu akizungumzia zoezi la chanjo ya Polio
wajumbe wa kikao wakichangia namna ya ufanikishaji wa zoezi la chanjo ya polio

Akitoa  taarifa  kwa  Kaimu  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa, Mwakilishi  kutoka  Wizara ya Afya   Christopher  Msaghae  amesema  kuwa  Wilaya  tayari  imepokea  Chanjo ya Polio zaidi  ya dozi  laki mbili kwa  ajili ya utekelezaji wa  zoezi  hilo

Sauti ya Christopher Msaghae kutoka wizara ya afya

Kwa  Upande wake Kaimu  Mkuu  wa  Wilaya ya  Maswa  ambaye  ni  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Itilima  Mhe  Anna  Gidarya  amesema  kuwa  zoezi  hili  lihusishe  viongozi  wa  ngazi  za chini  wakimo wenyeviti wa  vijiji  na  vitongoji na mabalozi ili  kuondoa  Upotoshaji   huku  suala  la  kutoa  elimu ya faida  ya  chanjo  hiyo  kabla ya  kuchanja  akilisisitiza  zaidi

Sauti ya Mhe Anna Gidarya kaimu dc maswa akizungumza wakati wa kikao hicho

Baadhi ya  wajumbe wa kikao hicho, Shekhe  wa Wilaya ya Maswa  Shehke Issa  Eliasa, katibu wa   waganga wa Tiba asili ndugu Potini Shiri  na  mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo Maswa  Bi Caroline Shayo  wakaahidi  kutoa  ushirikiano  wakati wa  utekelezaji wa  zoezi la utoaji wa  chanjo  hiyo

Sauti ya wajumbe wakitoa maoni yao ili kufanikisha zoezi la chanjo

Kikao   hicho kimehudhuriwa  na  wawakilishi wa  makundi mbalimbali wakimo,  Viongozi  wa  Dini, viongozi wa  tiba  asili, Wazee maarufu , makundi maaalumu,  walimu  wakuu, kamati ya  afya ya  msingi ya wilaya  na  viongozi wa kisiasa

Picha za wadau mbalimbali wakiwa katika kikao cha uhamasishaji wa chanjo wilayani Maswa