Sibuka FM

RC Nawanda apiga marufuku uuzaji wa vyakula mashuleni Simiyu

9 January 2024, 1:17 pm

Pichani Aliyesimama ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda akizungumza katika maeneo mbalimbali mkoa hapo katika kukabiliana na kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu Picha na Daniel Manyanga

Marufuku uuzaji wa vyakula mashuleni pamoja na kula vyakula maeneo yenye mikusanyiko ya watu ili kujikinga na kuenea kwa mlipuko wa magonjwa ya Kuhara na Kutapika.

Na,Daniel Manyanga

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda amepiga marufuku uuzaji wa vyakula mashuleni  pamoja na ulaji wa vyakula vya msibani lengo ni kupambana na kukabiliana kuenea kwa magonjwa ya mlipuko mkoani hapo ikiwemo Kipindupindu.

Marufuku  hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa kesi za watu kufariki na wengine kuuguwa ugonjwa wa Kutapika na Kuhara mkoani hapo hali ambayo imepelekea kufungwa kwa baadhi ya shughuli za kijamii ikiwemo minada inayokusanya watu wengi hali ambayo inaweza kusababisha watu kuweza kuambukizwa magonjwa hayo.

Dkt.Nawanda akizungumza na Watendaji,Maafisa afya na Wananchi  kwa nyakati tofauti tofauti mkoani hapa amesema kuwa hataki kusikia kesi za watu wamepata magonjwa ya  mlipuko mkoani hapo hali ya kwamba kuna njia za kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu mkoani hapa.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda akizungumza na Watendaji na Maafisa afya katika kukabiliana na kuenea kwa magonjwa ya milipuko pamoja na Sauti ya mratibu wa elimu ya afya kwa umma wilaya ya Maswa Bi.Salima Mahizi akizungumza namna ambavyo magonjwa haya wameathiri wilaya hiyo

Katika hatua nyingine Dkt.Nawanda amewataka Watendaji wote na Maafisa afya kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba ili kubaini nyumba ambazo hazina vyoo na kaya ambazo zikipatikana hazina vyoo faini yake ni shilingi 50,000/=

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda akiwataka watendaji kufanya misako ya nyumba kwa nyumba kukagua vyoo ili kukabiliana na mlipuko huo na kaya itakayokutwa na haina choo faini yake ni kiasi cha shilingi 50,000/=
Picha mbalimbali za maafisa afya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wakiendelea kutoa elimu na kusimamia usafi wilayani hapo ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu