Sibuka FM

18 wagundulika na kipindupindu Maswa,  mmoja afariki dunia

1 November 2023, 11:52 am

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Halmashauri ya wilaya ya Maswa Bi. Salma Mahizi akiwa Radio Sibuka fm kuzungumzia uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu

Na Nicholaus Machunda

Watu  18 wamegundulika  na  ugonjwa  wa  kipindupindu wilayani  Maswa  mkoani  Simiyu  huku  mmoja akifariki dunia  kutokana  na  ugonjwa  huo.

Hayo  yamesemwa  na  Mratibu  wa  Elimu  ya  Afya  kwa  Umma   Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Bi, Salma  Mahizi  wakati  akitoa  elimu  juu  ya  uwepo  wa  mlipuko  wa  ugonjwa  wa  kipindupindu na  namna  ya  kuchukua  tahadhari  kupitia  Radio  Sibuka  fm.

Bi  Mahizi amesema  kuwa   wagonjwa  wa  kwanza  kugundulika  walitokea  kijiji  cha  Sayusayu  kilichopo  kata  ya  Buchambi   ambapo  hadi  sasa  zaidi  ya  wagonjwa  18  wamegundulika  na  kati  ya  hao  mmoja  amefariki  dunia.

Sauti ya Salma Mahizi akizungumzia ugonjwa wa kipindupindu

Amesema  ugonjwa  wa  kipindupindu  ni  hatari  ambapo  baadhi  ya dailili zake   ni pamoja  na  kuharisha  na  kutapika  hali  inayopelekea mwili  kuchoka  na kukosa  nguvu na hatimae  kifo.

Sauti ya Salma Mahizi akizungumzia ugonjwa wa kipindupindu

Aidha  mratibu  huyo amesema kuwa halmashauri  imeweka  mikakati madhubuti  ili  kuhakikisha  mlipuko  huo  wa  kipindupindu  unadhibitiwa  usiendelee  kuenea katika maeneo  mengine  pamoja  na  kuimarisha  sehemu za  huduma  za  afya.

Sauti ya Salma Mahizi akizungumzia Ugonjwa wa kipindupindu