Sibuka FM

Wanawake jamii ya kihadzabe Meatu waomba msaada wa Rais Samia

1 March 2024, 5:03 pm

Jamii ya kihadzabe  inayoishi pembezoni mwa pori la hifadhi Makao Wilayani Meatu Mkoani Simiyu yahofia kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Pichani:Jamii ya Kihadzabe wakiwa Studio kushoto Saimoni Salehe,katikati ni Bi,Shuli Mujulu na Bi,Weyeweye

Na,Alex Sayi

Wanawake wa jamii ya kihadzabe wamuomba Rais Dkt,Samia kulinusuru kabila hilo ili lisiweze kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Hayo yamesemwa na kina mama jamii ya kihadzabe Bi,Weyeweye Khakhaha na Bi,Shuli Mujuli walipokuwa wakizungumza na Radio Sibuka fm.

Sauti ya Bi,Weyeweye Kakhaha

Weyeweye ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko hayo wanawake wa Jamii hiyo kwa sasa wanalazimika kuolewa na makabila mengine hali inayowawia ugumu kuyazoea mazingira hayo.

Sauti ya Bi,Weyeweye Kakhaya

Kwa upande wake Bi,Shuli Mujulu amesema kuwa kwa sasa wanashindwa kupata vyakula vyao vya asili  ikiwemo Matunda, Asali, Mizizi na Nyama hasa Nyama ya Nyani.

Pichani:Bi,Shuli Mujuli akiwa Studio
Sauti ya Bi,Weyeweye Kakhaya.