Sibuka FM

TEHAMA mashuleni kuongeza ufaulu kwa wanafunzi Maswa

26 April 2024, 4:24 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge mwenye suti nyeusi akimkabidhi kompyuta mpakato mwalimu mkuu shule ya msingi Binza Picha na Paul Yohana

Vifaa vya tehama sasa kusaidia ujifunzaji kwa wanafunzi shuleni nakuwasaidia walimu kwendana na wakati uliopo kwa sasa wa sayansi na teknolojia hivyo kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Na,Paul Yohana  
Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge amekabidhi vifaa vya tehema kwa maafisa elimu kata na wakuu wa shule ambavyo vitatumika mashuleni ili kuongeza ujuzi kwa wanafunzi na kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Aswege Kaminyoge amesema kuwa  vifaa hivyo vina gharama kubwa hivyo basi wanatakiwa kuvitunza kama mboni ya jicho kwa kushirikiana na maafisa elimu na wakuu wa shule ili viweze kudumu na kuleta tija kwa wanafunzi ambao wanaenda kuvitumia haswa kwenye kuongeza ufaulu.

Sauti ya Dc Maswa akizungumza wakati wa kukabidhi

Vivian Christian ni kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa amesema kuwa vifaa hivyo wamevipokea kutoka mkoani na vitapelekwa kwenye shule mbili za Binza na Malampaka  na kutaja  vifaa hivyo ni kompyuta mpakato (4) smart tv mbili  inch 65 pamoja na kamera 2.

Sauti ya kaimu mkurugenzi mtendaji Vivian Christian

Kwa upande wake afisa elimu msingi wilaya ya Maswa Dkt.Lucy Kulongw’a amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia katika kuongeza ujifunzaji kwa wanafunzi hivyo basi wakuu wa shule wakavitumie huko mashuleni na siyo kuviweka ndani kama mapambo.

Sauti ya afisa elimu msingi akiwataka walimu kuvitumia vifaa hivyo kwa dhumuni lililokusudiwa