Sibuka FM

Miti million moja na nusu kurejesha uoto wa asili Maswa

30 April 2024, 7:04 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiwa ameshika mti tayari kwa upandaji Picha na Paul Yohana

Maswa kurejesha uoto wa asili kwa zoezi endelevu la upandaji miti ili kuhakikisha wilaya inatunza vyanzo vya maji nakuifanya Maswa kuwa ya kijani.

Na,Poul Yohana

Halmashauri ya wilayani Maswa mkoani Simiyu imepanda miti 252 katika jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Binza ili kuendelea kulinda mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia pamoja na ukame.

Akizungumza na Sibuka fm wakati wa zoezi la upandaji miti afisa mazingira wilaya ya Maswa,Dutu Lubinza amesema kuwa mpaka sasa wamefikia asilimia arobaini na tano ya upandaji wa miti kati ya mil,1.5 ambayo unatarajiwa kupandwa huku zoezi hilo likiwashirikisha wadau mbalimbali wilayani hapo.

Sauti ya afisa mazingira akizungumzia mpango wa kupanda

Lubinza ameongeza kuwa ili kuhakikisha zoezi linakuwa endelevu wananchi wanapaswa kuhakikisha wanatunza miti yote iliyopandwa ili kurejeshea uoto wa asili hali ambayo itasaidia katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Sauti ya afisa mazingira akitoa wito kwa wananchi kutunza miti na kupanda

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Binza ,Joseph Mgeta amesema kuwa miti hiyo itakuwa na faida kwa wanafunzi kwani watapata vivuli na kuni.

Sauti ya mwalimu mkuu shule ya msingi Binza