Sibuka FM

Maswa: Wafugaji waaswa kushiriki  utunzaji mazingira, vyanzo vya maji

15 August 2023, 3:30 pm

Pichani:Baadhi ya wafugaji wakiwa wameketi kwenye moja ya Mabirika yakunyweshea Mifugo kwenye kikao cha Wafugaji na Mkuu wa Wilaya.Picha na Alex Sayi.

Wafugaji Wilayani Maswa Mkoani Simiyu watakiwa wawe sehemu ya uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya Maji.

Na,Alex Sayi.

Wafugaji Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wameaswa kushiriki utunzaji wa Mazingira na  vyanzo vya Maji kwa kutokupeleka mifugo  kwenye chanzo kikuu cha Maji  cha Bwawa la New Sola kinachotegemewa na wakazi Wilayani hapa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge wakati akizungumza na baadhi ya wafugaji katika kijiji na Kata ya Zanzui Wilayani hapa ili kubaini changamoto zinazowakabili wafugaji hao.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Aswege Kaminyoge.
Pichani: Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge mwenye Kofia mkononi akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya Wafugaji,nawa pili kushoto ni Diwani wa kata hiyo Jeremia Makondeko.Picha na Alex Sayi.

Mayenga Sangalali mfugaji na mkazi wa Zanzui Wilayani hapa amesema kuwa wafugaji walishindwa kuendelea kunywesha mifugo yao kwenye mabirika kutokana na gharama kuwa kubwa.

Sauti ya Mayenga Sangalali mmoja wa Wafugaji.

Msimamizi wa moja ya mabirika katani hapa toka Mamlaka ya Maji  na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA)amesema kuwa wafugaji walishindwa kulipia Sh.40 kwa kila kichwa cha Ng’ombe.

Sauti ya msimamizi wa Mabirika yakunyweshea mifugo toka (MAUWASA)

Kaminyoge akitolea ufafanuzi wa gharama za unyweshaji kwenye mabirika hayo  amesema kuwa wameshawasiliana na (Ewura) na wamekubaliana kushusha bei hiyo hadi Sh.20

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Kaminyoge

Diwani wa Kata hiyo Jeremia Shigala Makondeko amesema kuwa anamshukuru Rais Samia kwakuendelea kuwasogezea huduma za kijamii wananchi wa Kata hiyo huku akiwaasa wafugaji wa Kata hiyo kujenga desturi ya kupanda miti ya mbao na matunda ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Baadhi ya mifugo ikiwa malishoni.