Sibuka FM
Sibuka FM
5 May 2025, 14:46

Ninatangaza rasmi kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bariadi Vijijini endapo Rais ataridhia kupitia Tume huru ya Uchaguzi Jimbo kugawanywa na kuwa mawili (Bariadi Mjini na Bariadi Vijijini) basi mimi nitagombea vijijini “Mhandisi Kundo Mathew “
Mbunge wa Jimbo la Bariadi na Naibu waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew ametangaza rasmi kugombe nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bariadi vijijini endapo mchakato wa kuligawa jimbo hilo utakamilika
Mhandisi Kundo ametangaza dhamira hiyo wakati wa Uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi –ccm ya 2020/2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa ccm katika Jimbo la Bariadi uliofanyika katika shule ya Msingi Bariadi alliance
Aidha Mhandisi Kundo amesema kuwa katika utekelezaji wa Miaka mitano ya Ilani ya ccm , Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan imefanya mambo makubwa katika Sekta za Afya, Elimu, Maji, Barabara , Umeme na Kilimo ukilinganisha na hapo awali wakati anachaguliwa kuwa mwakilishi wa Wananchi katika Jimbo hilo

Leila Burhan ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya ccm Taifa ndiye alikuwa Mgeni rasmi , amewaomba wana Bariadi kumuunga mkono na kuumpa sapoti Mhandisi Kundo muda utakapofika wa kwenda kugombea Ubunge kwa Jimbo lolote katika Wilaya ya Bariadi
Akimkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Simiyu Ndugu Shemsa Mohamed amesema kuwa kwa masrahi mapana ya Bariadi wameomba Jimbo ligawanywe ili kusogeza huduma kwa wananchi kwani kwa sasa Jimbo lina kata 31 hivyo ni kubwa mno katika kulihudumia
Akitoa salamu za Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Kenani Kihongosi amesema kuwa Mkoa umepokea Fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa
