Sibuka FM

Wakulima wafundwa kuhusu teknolojia za kisasa kuongeza uzalishaji

8 August 2024, 21:54

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Kanali Evans Mtambi akiongea katika kilele cha maonesho ya Siku ya Wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. Picha Nicholaus Machunda.

Na Nicholaus Machunda – Simiyu

Wananchi  wa  Mikoa  ya  Shinyanga ,  Simiyu na  Mara wameaswa  kutumia  teknolojia ya kisasa ya  kilimo ili kujikwamua kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe, Kanali Evans Alfred Mtambi ambaye alikuwa  Mgeni rasmi katika  kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima maarufu kama Nanenane.

Sauti ya RC Mara Mh. Kanali Evans Mtambi wakati wa kilele cha maonesho ya Nanenane

Aidha Mh. Mtambi amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa  mitatu inayounda Kanda ya Ziwa  Mashariki  kukutana mara moja ili kuanza mipango ya kuandaa miundombinu ya msimu ujao  ili  kuwe  na  Maonyesho  yenye  tija  kwa  Wakulima na  wafugaji.

Sauti ya RC Mara Mhe Kanali Evans Mtambi wakati wa kilele cha Maonesho ya Nane nane

Akimkaribisha  Mgeni  rasmi,  Mkuu  wa  Mkoa   wa  Simiyu  ambaye  ndio  mwenyeji  wa  Maadhimisho  hayo  Mhe,   Kenani  Laban  Kihongosi   amesema   kuwa  ifike   wakati  wakulima  wabadilike    katika   kutumia  mbinu  na  Zana  Bora  za kilimo.

Sauti ya RC Simiyu Mh Kenani Kihongosi wakati wa Nane nane Nyakabindi – Bariadi

Naye  Mkuu wa Mkoa  wa Shinyanga Mhe,  Anamringi  Macha  amewataka   wakulima  na  Wafugaji  mikoa  ya  Kanda  ya  ziwa  Mashariki (Mara, Simiyu na Shinyanga ) waendelee kuja  katika viwanja vya Nyakabindi ili kunifunza zaidi.

Sauti ya RC Shinyanga Mhe Anamringi Macha

Akitoa  salamu  za  Chama, mwenyekiti  wa  chama  cha  Mapinduzi   Mkoa  wa  Mara  Ndg.  Patrick  Chande  Marwa   amewapongeza   wandaaji  wa  sherehe  hizo na kuwaomba  waongeze  ubunifu ili mwakani   yafae  zaidi.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndugu Patrick Marwa- Salamu za chama

Kauli  mbiu  katika   sherehe  za  Wakulima  Nane  nane  kwa  mwaka  huu  2024  ni  Chagua Viongozi  Bora wa  Serikali za  Mitaa  kwa  Maendeleo  Endelevu  ya Kilimo, Mifugo  na  Uvuvi.