Sibuka FM

Maswa:Halmashauri maswa yazindua mnada mpya

3 March 2025, 12:36

Pichani:Kushoto ni mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Wilaya ya Maswa Mh,Paul Maige ,akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Bw,Maisha Mtipa na mwisho kulia ni Bw,Charles Kilapilo.Picha na Neema Solo.

Halmashauri Wilayani Maswa Mkoani Simiyu imeendelea na adhima yake ya kuhakikisha inaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kuanzisha vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuharakisha maendeleo Wilayani hapo

Na, Alex Sayi-Maswa Simiyu.

Halmashauri wilayani Maswa mkoani Simiyu imeanzisha gulio na mnada mpya wa mifugo kwa lengo la kuchochea maendeleo kwa wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw,Maisha Mtipa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la robo ya pili,lilioketi feb,27/2025.

Pichani:Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Bw,Maisha Mtipa.Picha na Neema Solo
Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Maswa,Bw.Maisha Mtipa

Aidha akizindua mnada huo katibu tawala wa Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu,Bw,Athuman Kalaghe amewapongeza madiwani kwa uamuzi huo,huku akitoa maelekezo juu ya usimamizi wa mnada huo

Pichani:Anaezungumza ni Katibu Tawala Wilaya ya Maswa Bw,Athuman Kalaghe akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa chama Tawala na baadhi ya watumishi wa Halmashauri siku ya uzinduzi wa mnada mpya uliozinduliwa rasmi feb,28/2025.Picha na Neema Solo
Sauti ya Katibu Tawala Wilaya ya Maswa,Bw,Athuman Kalaghe

Kwa upande wake  mkuu wa divisheni ya kilimo na uvuvi,Bw,Robert Urasa amesema kuwa mnada huo umegharimu zaidi ya Sh.Mil,34

Sauti ya Mkuu wa Divisheni ya Kilimo na Uvuvi,Robert Urasa
Pichani:Mkuu wa Divisheni ya kilimo na Uvuvi Bw,,Robert Urasa akisoma taarifa ya uanzishaji wa mnada mpya Feb,28/2025.Picha na Neema Solo.