Sibuka FM

Mwarobaini kwa wanaochezea mizani ya kupimia pamba wapatikana

22 May 2026, 18:02

Pichani (aliyesimama ameshika karatasi )ni Penina Range afisa kilimo Bodi ya Pamba kitengo cha Usafi na Ubora wa Pamba akifafanua jambo kuhusu utunzaji, usafi na ubora wa pamba katika kijiji cha Dutwa Wilayani Badiadi Mkoani Simiyu. Picha na Nicholaus Machunda

Hatutawavumilia viongozi wote watakaofanya udanganyifu wa uchezea (kuchakachua) mizani kwa lengo la kuwaibia wakulima, Lakini pia hatutawavumilia wakulima wataoharibu pamba kwa kuweka Maji, mchanga au Mafuta ya kenge hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufungwa Jela. “Ndinda Antony – Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi

Serikali  kupitia  Bodi ya Pamba  Tanzania  –TCB  imekuja  na  suluhisho kwa  wanaochezea  mizani  ya  kupimia  pamba  kwa  lengo la kuwaibia  wakulima  wa zao  hilo  maana  nia  ya Serikali  ni  kuinua  kipato cha  mkulima mmoja  na   taifa  kwa  ujumla

Hayo yamesemwa  na  mkaguzi wa pamba Wilaya ya  Bariadi  Mkoa  wa  Simiyu  ndugu  Ndinda  Antony  wakati  akiongea  na  viongozi  wa  Amcos  katika kata ya  Dutwa wilayani hapo  wakati  wa utoaji wa wa Semina  ya usafi na ubora wa pamba iliyoandaliwa na bodi ya Pamba  Tanzania

hii hapa ni sauti ya Ndinda Antony Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi akizungumza na viongozi wa Amcos -Dutwa

Ndugu  Ndinda  ameongeza  kuwa  katika kuhakikisha  ubora  wa  pamba unasimamiwa, sheria ipo wazi wa  wataofanya  udanganyifu wa  kuweka  maji, kuweka michanga  au  mafuta ya  kenge  kwenye pamba watachukuliwa  sheria  ikiwemo  kufungwa jela  au  kulipa  faini au vyote  kwa  pamoja

bonyeza haa kusikiliza sauti ya Ndinda Antony Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi
Ndinda Antony mkaguzi wa Pamba wilaya ya Bariadi akizungumza na viongozi wa Amcos kata ya Dutwa

Kwa  upande  wao maafisa kilimo wa program ya Jenga kesho  iliyo bora – BBT  wamesema  watatumia  vyema   taaluma na  maarifa yao waliyopata  kwa  kuwashauri vyema wakulima  kufuata  kanuni bora za  kilimo ikiwemo  uvunaji sahihi wa  pamba  ili kuweza  kuthibiti ubora  wa  pamba

sauti za baadhi ya maafisa kilimo wa BBT wakizungumza baada ya kupata mafunzo ya usafi na ubora wa Pamba

Nao  baadhi ya  viongozi wa  AMCOS  walioshiriki mafunzo hayo ya  Usafi na  ubora  wa  Pamba  kutoka  wataalamu wa maabara kitengo cha usafi na ubora wa pamba wamesema  wataenda  kusimamia  kikamilifu ubora  wa  pamba kwa  kufuata  sheria, kanuni  na  maagizo waliyopewa

sauti za baadhi ya viongozi wa Amcos wakizungumza baada kuapata mafunzo ya namna ubora wa pamba

Bodi ya  Pamba  Tanzania  kupitia  maafisa wa kitengo cha maabara na  usafi  wa pamba  wanapita  katika maeneo mbalimbali  ya  mikoa  inayolima  zao hilo la  pamba  kwa lengo la kutoa  elimu  ya  utunzaji, Usafi na  ubora  wa  Pamba.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Renatus Luneja akizungumza na viongozi wa Amcos kata Dutwa- Bariadi