Sibuka FM

Kondoo, mbuzi 33 wauliwa na chui Simiyu

11 November 2025, 10:43

Muonekano wa mnyama Chui akiwa juu ya mti akipata kitoweo baada ya kufanikisha mawindo yake. Picha kwa msaada wa mtandao

Tulianza na matukio ya  Fisi kushambulia mifugo ya wananchi katika baadhi ya maeneo mkoani Simiyu na sasa hivi Chui nao wanapita mule mule kuwatia hasara wananchi kwa akili yangu tu ndogo najiuliza hizi hasara nani anazilipa maana kama kuna mamlaka husika za wanyama zipo na bado hasara ipo kwa wafugaji”.

Na, Daniel Manyanga 

Chui dume ambaye ni miongoni mwa waliouwa Kondoo na Mbuzi 33 wa wananchi wa kijiji cha Mwalali kilichopo kitongoji cha Chungu cha Ntemi  kata ya Mwaswale wilayani Itilima mkoani Simiyu nchini Tanzania  wanaswa kwenye mtego uliowekwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na anasafirishwa kupelekwa kwenye mashamba ya serikali huku wengine watatu wakiwemo chui jike na watoto wawili nao wakiwekewa mtego ili kuondoa usumbufu na hasara kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wakizungumza na Sibuka Fm, Salu Ntuguto na Sanilo Kadaso wakazi wa kijiji cha Mwalali wamesema kuwa uwepo wa wanyama hao umekuwa ukiwasumbua wananchi wa maeneo hayo hasa kuvamia na kuua mifugo yao nyakati tofauti hivyo wameziomba mamlaka zinazohusika na wanyama kuona namna nzuri ya kuwaondoa chui hao kwenye maeneo yao ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Sauti ya wananchi wa kijiji cha Mwalali

Huja Huja ni mkazi wa kijiji hicho amesema kuwa uwepo wa wanyama hao kumewatia hasara ya kuliwa kwa mifugo yao.

Sauti ya Huja Huja mmoja ya wakazi wa kijiji hicho akielezea namna ambavyo mnyama chui alivyowatia hasara

Kwa upande wake  mwenyekiti wa kijiji hicho, Balida Nandi amesema siku za nyuma chui aliwahi kuchukua mbuzi majira ya saa kumi jioni na kuingia naye mlimani huku baadhi ya wananchi wakishuhudia kwa macho.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Mwalali, Balinda Nandi akizungumzia matukio ya chui kuvamia na kuua makundi ya mifugo

Baadhi ya vijiji vilivyopo wilaya ya Itilima vinazungukwa na pori la akiba Maswa kama ilivyo vijiji vilivyopo  wilaya za Meatu na Bariadi mkoani hapa kama anavyofafanua Dkt.Elias Mwamsabe daktari wa wanyamapori kutoka TAWA

Sauti ya Dkt.Elias Mwamsabe kutoka TAWA