This image has an empty alt attribute; its file name is rpc.jpg
Sibuka FM

Watatu wakutwa wamekufa kwa kunyongwa wakiwemo watoto wawili Itilima

11 August 2023, 7:38 pm

This image has an empty alt attribute; its file name is rpc.jpg
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe akizungumza na eaandishi wa habari. Picha na Daniel Manyanga

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linamtafuta mke wa marehemu kufuatia vifo vya watu watatu akiwemo mme wa marehemu na watoto wawili vifo hivyo vimetokana na kunyongwa.

Na,Daniel Manyanga

Watu watatu wamekutwa wamekufa kwa kujinyonga katika kata ya Kinamweli kijiji cha Mwantemi wilayani Itilima Mkoani Simiyu katika tukio hilo la kutisha lililotokea mnamo tarehe 11.08.2023

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP,Edith Swebe amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.08.2023 majira ya saa 07:00 asubuhi ambapo  miili ya watoto wawili ilikutwa imening’inizwa kwenye chumba wanacholala na wazazi wao huku uchunguzi ukionesha wamekufa kwa kunyongwa.

ACP Swebe ameongeza kuwa mwili wa mtu wa tatu aitwae Bundu Ng’habi mwenye miaka 32 ,Msukuma na mkulima ambaye pia ni baba mzazi wa watoto waliokufa kwa kunyongwa ulikutwa ukiwa umening’inia juu ya mti kwa kujinyonga .

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la polisi ACP ,Edith Swebe

Aidha ACP Swebe amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mke wa marehemu ambaye mpaka sasa hajulikani alipo ili kuweza kusaidia uchunguzi juu ya tukio hilo.

Sauti ya ACP,Swebe kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za migogoro ya kifamilia ili kuweza kupatiwa ufumbuzi wa migogoro kwa kushirikiana na serikali za mitaa na viogozi wa dini ili kujiepusha na migogoro isiyo kuwa yalazima.