Sibuka FM

DC Anney watumishi wa afya fanyeni kazi kwa weledi

11 November 2025, 11:23

Picha ya pamoja ikimuonesha mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Vicent Anney mwenye suti nyeusi akiwa na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na chama wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la X-Ray. Picha na Samwel Mwanga

Hakuna maendeleo ya vitu bila watu ndiyo maana sasa duniani kote wanapambana sana kuleta ustawi wa afya za watu wakijuwa kabisa kwamba watu wakiwa na afya imara hata uchumi nao utakuwa kwa kasi kwa sababu tu wananchi wake wako na afya na nguvu kufanya kazi za kiuchumi”.

Na, Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu nchini Tanzania, Dkt. Vicent Naano Anney amewataka watumishi wa kituo cha afya cha Barikiwa mjini Maswa kinachomilikiwa na mzawa wa mjini hapo, Dkt. Ashrey Lucas  kufanya kazi kwa weledi katika kuwahudumia wananchi wanaokuja kupata huduma mbalimbali za matibabu kituoni hapo.

Kwenye picha ni mkuu wa wilaya ya Maswa,Dkt.Vicent Naano Anney akizungumza jambo na hadhara iliyohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi jengo la X-Ray katika kituo cha afya Barikiwa. Picha na Samwel Mwanga

Dkt. Anney amesema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika  jengo la X-Ray katika kituo hicho ili kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za matibabu kwa wananchi pamoja na kupunguza gharama za kufuata huduma hiyo sehemu nyingine.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akiwataka wafanyakazi wa kituo cha afya Barikiwa kufanya kazi kwa weledi
Kwenye picha aliyekaa mbele ni mkurugenzi wa Barikiwa Health Center, Dkt.Ashrey Lucas akifatilia jambo kwa umakini mkubwa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la Xray Picha na Samwel Mwanga

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha afya cha Barikiwa ,Dkt.Ashrey Lucas amesema kuwa wataendelea kuleta madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali hapa nchini katika kutoa huduma za kibingwa huku mganga mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt. Hadija Zegega amemshukuru Dkt. Ashrey kwa uwekezaji huo ambao unasaidia wananchi kupata huduma bora za matibabu kwa ushirikiano na serikali.

Sauti ya mkurugenzi wa Barikiwa Health Center na mganga mkuu wa wilaya ya Maswa wakizungumza jambo
Kwenye picha ni mganga mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Hadija Zegega akizungumza jambo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo la X-Ray. Picha na Samwel Mwanga

Jamali Mtende na Bertha Machama ni baadhi ya wanufaikaji wa kituo hicho cha afya waliopatiwa matibabu wameshukuru kwa namna ambavyo kituo hicho kinavyotoa huduma za kibingwa kwa nyakati tofauti hivyo kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hizo sehemu zingine.

Sauti ya baadhi ya wanufaikaji wa matibabu katika kituo hicho cha afya cha Barikiwa