Sibuka FM

Itilima wakosa huduma ya maji safi na salama kwa wiki tatu

16 April 2024, 7:32 pm

Pichani ni wananchi wakiwa wamekinga maji ya bomba katika kijiji jirani kufuatia mota kuungua.Picha na Daniel Manyanga

Watembea umbali wa kilomita 3 kufuata huduma ya maji safi na salama kufuatia mota ya kusukuma maji kuungua kijijini hapo.

Na. Daniel Manyanga 

Wananchi wa vijiji vya Mlimani na Zanzui vilivyopo  wilayani  Itilima mkoani Simiyu  wakosa huduma ya maji safi na salama  ya bomba kwa muda wa wiki tatu kufuatia  mota ya kusukuma maji kuungua  hatua iliyopelekea kupata huduma hiyo  kijiji jirani  cha Kabale kilichopo  umbali wa kilomita tatu kutoka kwenye vijiji hivyo.

Akizungumza na Sibuka Fm ilipofika kijijini hapo kwa lengo la kujionea adha wanayopitia hivi sasa, wananchi hao mwenyekiti wa kijiji cha Zanzui Ndg. Michael Mabula amesema kuwa kuungua kwa mota hiyo ambayo husukuma maji katika vijiji hivyo wananchi  wamepata changamoto kubwa hali ambayo imewafanya kupata huduma ya maji safi na salama kutoka kijiji kingine kilichopo umbali wa kilomita 3.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Zanzui akizungumzia adha wanayoipata wananchi wake kutokana na kuungua kwa mota.

Kwa upande wake meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa  Mazingira vijijini RUWASA wilaya ya Itilima Hussein Yahaya amesema kuwa tayari wameshachukua hatua za kurejesha huduma hiyo muhimu kwa wananchi katika maeneo hayo.

Sauti ya meneja RUWASA akizungumzia hatua walizozichukua mpaka Sasa kurejesha huduma ya maji.
Picha katika matukio mbalimbali zikionesha wananchi wakiwa wanasubiri kuchota maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali