Sibuka FM

TRA yatoa mafunzo ya Elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara Maswa

24 September 2026, 20:27

Picha. Aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Vicent Anney, kushoto kwake ni John Chagu- mwenyekiti wa Wafanyabiashara Maswa na Kulia ni meneja wa TRA wilaya ya Maswa wakiwa katika kikao na wafanyabiashara( hawapo pichani ) Picha na Nicholaus Machunda

Hakuna Nchi yoyote Duniani inayofanya maendeleo bila kulipa Kodi, Hivyo niwasihi wafanyabiashara wenzangu tulipe kodi kwa wakati na kwa Uzalendo ” John Chagu – Mwenyekiti wa wafanyabiashara “

MamlakayaMapata Tanzania TRA  Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imeendesha mafunzo ya Elimu ya Kodi na masuala yanayohusiana na ulipaji wa Kodi kwa Wafanyabiashara na Wajasiliamali wilayani hapa.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe,  Dkt Vicent Naano Anney amesema kuwa wafanyabiashara wengi hawatoi rist ya mashine ya  EFD  hali inayopelekea kutokuwa na kumbukumbu za  bidhaa na mauzo kwa mfanyabiashara hivyo kuwataka kuwaWazalendo katika ulipaji wa Kodi.

sauti ya Mhe Vicent Anney – DC Maswa
Afisa Elimu na Mawasiliano kutoka TRA Mkoa wa Simiyu Benjamin Makobwe akitoa elimu ya masuala ya Kodi kwa wafanyabiashara na wajasiliamali wa Mji wa Maswa..

Aidha Mhe Anney amewataka wafanyabiashara kuwa wabunifu ili kuleta ushindani wa Bidhaa kwani sekta binafsi inamchango mkubwa katika kutekeleza Dira ya Maendeleo 2050  huku akiwataka kuwa wafuatiliaji wa mabadiliko ya sharia ya kodi ili kuepuka kuingia mgogoro na serikali

sauti ya DC maswa Mhe Vicent Anney akizungumza na wafanyabiashara mji wa Maswa
Meneja TRA Wilaya ya Maswa Kisaro Focus

Kwa Upande wake Meneja wa  TRA Wilaya ya Maswa Kisaro Fucus amesema lengo la  kuwakutanisha wafanyabiashara hao ni kuwahimiza utoaji wa risti na matumizi sahihi ya mashine za EFDs, kuwapitisha kwenye mabadiliko ya sharia za kodi kwa mwaka wa fedha  2026/2027 pamoja na kuwakumbusha ulipaji wa Kodi ya Mapato kwa awamu ya tatu.

hii hapa sauti ya Meneja wa TRA Wilaya ya Maswa Kisaro Focus

Naye mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Maswa ndugu  John  Chagu kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake ameishukuru TRA kwa kutoa elimu ya masuala ya Kodi na kuongeza kuwa  hakuna  Taifa linalofanya maendeleo bila kulipa Kodi hivyo wafanyabiashara wawe wazalendo kwa kulipa Kodi sahihi na kwa wakati

hii hapa sauti ya John Chagu – mwenyekiti wa wafanyabiashara Maswa
Ndugu John Chagu akizungumza na wafanyabiashara wenzake kuhusu Umuhimu wa kulipa Kodi