Sibuka FM

Wawili wafariki dunia wakisafisha kisima Bariadi

14 November 2026, 16:15

Pichani ni kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Faustin Mtitu akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio la vifo vya watu wawili kutokana na kutumbukia kwenye kisima Picha kutoka maktaba ya Sibuka FM

“Ni kweli katika utafutaji wa maisha huwezi kubagua kazi ipi ya kufanya lakini tufanye basi kazi ambazo tunaziweza zisizo na uhatari wa maisha yetu kama huna ujuzi nayo waachie wenye utalaamu huo”.

Na Daniel Manyanga 

Watu wawili waliofahamika kwa majina ya Bahame Simiyu (45) na Kimola Nsulwa (23) wote wakazi wa mtaa wa Katenga kata ya Isanga wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye kisima walichokuwa wakikisafisa kwa ajili ya kufunga pampu za maji.

Wakizungumza na Sibuka Fm mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Amina Said na Holela Seme wanaeleza tukio lilivyokuwa hadi kupelekea umauti wa marehemu hao.

Sauti ya mashuhuda wa tukio hilo

Tukio hilo limeacha simamzi na pengo lisilozibika kwa familia za watu hao kama wanavyoeleleza Lucia Cheyo ambaye ni mama wa marehemu Kimola Nsulwa na Nshoma Masala ambaye ni mke wa marehemu Bahame Simiyu.

Sauti ya mzazi na mke wa marehemu

Naye diwani wa kata ya Isanga ,Nashon Ngussa na kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji ,Faustin Mtitu, wamewaasa wananchi kujiepusha na kazi hatarishi ambazo hawana ujuzi nazo na badala yake watumie watu wenye utaalam na kazi hizo ili kujiepusha na madhara yasiyokuwa ya lazima ambayo yanaacha makovu katika familia.

Sauti ya diwani na kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu