Sibuka FM
Sibuka FM
13 November 2026, 05:26

“Hatuwezi kuvumilia vitendo vya rushwa wala kuona kodi za watanzania wazalendo zinatumika isivyo kutokana na baadhi ya watumishi wa umma kuzifanyia ubadhilifu lazima sheria ichukuwe nafasi yake”.
Na,Daniel Manyanga
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU ) mkoa wa Simiyu imefanikiwa kuwarejeshea zaidi ya milioni 54 wakulima wa zao la pamba walikuwa wamedhulumiwa na AMCOS baada ya kununuliwa pamba yao kwa mkopo katika msimu wa mwaka 2026/27.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) mkoa wa Simiyu,Aron Misanga amesema kuwa kupitia oparesheni za uchunguzi walifanikiwa kuwarejesha wakulima fedha hizo kutokana na dhuluma iliyofanywa na AMCOS huku wakulima 68 wakilipwa fedha zao kabla ya msimu wa kilimo kuisha.
Naibu mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Simiyu, Aron Misanga amesema kuwa kupitia dawati la uzuiaji rushwa wamefanikiwa kuongeza mapato ya hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Itilima kutoka shilingi laki tano kwa mwezi hadi milioni 35 kuanzia mwezi June mwaka huu huku halmashauri ya mji wa Baridi TAKUKURU imefanikiwa kurejesha mifuko 370 ya saruji katika ujenzi wa jengo la watoto hospitali ya mji wa Bariadi.
Nkambi Abdallah na Mgaya Masunga ni baadhi ya wakazi wa mkoa wa Simiyu wameiomba TAKUKURU kuzuia vitendo vya rushwa hospitalini na vituo vya kutolea huduma ya afya vinavyosababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa hasa wasiokuwa na uwezo wa kifedha kutokana na baadhi ya matabibu kuangalia zaidi ulichonacho mkononi.