Sibuka FM

RC Mtanda waganga wa tiba asili fichueni wahalifu

17 September 2026, 12:01

Pichani mkuu wa mkoa wa Simiyu, Said Mtanda akiwa katika moja wapo wa shughuli za kiserikali. Mkoani hapo Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

“Katika shughuli zenu jitahidini sana kuwa walinzi wa amani katika jamii yetu kuweni sehemu ya kufichua uhalifu na wahalifu wenyewe na siyo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani”.

Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu ,Said Mtanda amewataka waganga wa tiba asili na mbadala mkoani humo kutumia vilinge vyao kufichua watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili wachukuliwe hatua kali za kisheria jambo litakalosaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii na siyo kupiga ramli chonganishi.

Mtanda ametoa wito huo wakati akizungumza na waganga wa tiba asili na mbadala wa mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi, ambapo amesema kuwakuna umuhimu mkubwa kwa kundi hilo kushiriki kikamilifu kufichua wahalifu ili kupunguza vitendo viovu ndani ya jamii zetu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Said Mtanda akizungumza na waganga wa tiba asili mkoani hapo

Awali akizungumza katika kikao hicho kaimu katibu wa waganga wa tiba asili mkoa wa Simiyu, Bunani Jackson ameeleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao na kuiomba serikali kuzifanyia kazi.

Sauti ya waganga wa tiba asili

Akijibia changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Simiyu, Said Mtanda akaeleza hatua zitakazofanywa na serikali ya mkoa huo katika kushughulikia changamoto za waganga hao.