Sibuka FM
Sibuka FM
16 September 2026, 06:14

“Tunahitaji usalama kwanza wa watu na mali zao ni kweli kabisa wanyama pori tunawahitaji sana katika kuongeza pato la taifa lakini kama usalama wa watu ni mdogo hiyo fedha ya utalii itakuwa na faida gani kama watu kila siku wanavamiwa na wanyama pori kwenye makazi yao”.
Na,Daniel Manyanga
Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuwadhibiti Tembo wasiingie kwenye maeneo ya makazi ya watu na kusababisha athari tofauti tofauti bado wakazi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wameiomba serikali iongeze udhibiti wa wanyama hao ili kuwaondolea hasara inayosababishwa na uharibifu wa mazao,makazi pamoja na maafa.
Wakizungumza na Sibuka Fm,Layi Madwani,Matondo Kweja na Mayanzi Lyang’ombe ambao ni wakazi wa vijiji vya Matongo,Mwauchumu, Ihusi na Mwasilimbi wamesema kuwa bado wanakumbana na changamoto ya wanyamapori kuingia kwenye maeneo ya makazi ya watu na kushambulia mazao yao.
Kwembea Senso ni afisa wanyamapori wa wilaya ya Bariadi ambaye ameeleza mwenendo wa matukio ya uvamizi wa wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo ya makazi ya watu na namna ambavyo wamejipanga kuzuia uvamizi wa wanyama hao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akatoa maelekezo ya serikali ili kuhakikisha wale wote waliopata athari za wanyamapori wanalipwa fidia wanazostahili.