Joy FM

Wakimbizi waaswa kuacha kukata miti kasulu

6 June 2024, 10:34

Wakimbiziwaishio katika kambi ya wakimbizi, Picha na Michael Mpunije

Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wakimbizi katika kambi ya nyargusu wilayani kasulu mkoani kigoma wametakiwa kutunza misitu inayowazunguka ili iweze kudumu na kutumia nishati safi ya kupikia ambayo haiathiri mazingira.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wakimbizi raia nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo waishio katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani kasulu mKoani Kigoma wametakiwa kujenga Tabia ya kupanda miti na kuacha matumizi ya Kuni na kuanza kutumia nishati mbadala ya kupikia ili kulinda mazingira.

Rai Hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Issac Mwakisu ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika jana katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ambayo yameambatana na Kauli mbiu isemayo “Ardhi yetu ,Kesho yetu”

Wakimbizi wa kambi ya wakimbizi nyarugusu wakiwa katika mkutano na viongozi, Picha na Michael Mpunije

Kanali mwakisu amesema ni wakati wa wananchi hao kukemea ukame katika maeneo hayo na kujikita katika mkakati wa kuhakikisha wanalinda mazingira ambayo ni chachu katika uhai wa mwanadamu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu kigoma

Aidha Kaimu Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Humphurey Mrema pamoja na Mkuu wa Shirika la UNHCR Kasulu John Bosco Mgomon wamesema watahakikisha Nyarugusu inaendelea kuwa katika mzingira bora kama yalivyo kwasasa kwani wenyeji na wakimbizi wamekuwa tayari katika kufanisha zoezi hilo.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Humphurey Mrema pamoja na Mkuu wa Shirika la UNHCR Kasulu John Bosco Mgomon

Kwa upande wao baadhi ya wakimbizi wamesema wataendelea kuyatunza mazingira ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.

Sauti ya wakimbi wa kambi ya nyarugusu