Joy FM

Uharibifu wa mazingira chanzo cha mabadiliko ya tabianchi

6 June 2024, 09:19

Afisa mazingira akizungumza na wananchi walihudhuria siku ya mazingira, Picha na Hamis Ntelekwa

Serikali imewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kusaidia kupunguza majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa.

Na Josphine Kiravu

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia utunzaji wa mazingira ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na ongezeko la mvua ambazo mara kadhaa zimekuwa zikiathiri makazi ya watu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira (NEMC) kanda ya magharibi Edgar Mgila wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kwa kusirikiana na Taasis ya Jane Goodall wamepanda miti katika shule ya sekondari ya Bitale.

Ni baadhi ya wanafunzi wakiwa na watalaamu wa mazingira siku ya mazingira duniani , Picha na Hamis Ntelekwa

Amesema hali inayoonekana kwa sasa ya kina cha maji ya ziwa Tanganyika kuongezeka ni matokeo ya uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya wananchi iwe kwa kujua ama kutokujua.

Sauti ya mkurugenzi wa baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira kanda ya magharibi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa sayansi ya uhifadhi kutoka Taasis ya Jane Goodall Dr Shedrack Kamenya amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ya uhifadhi wa mazingira kupitia miradi mbalimbali ikiwemo roots and shoots.

Sauti ya Mkurugenzi wa sayansi ya uhifadhi Jane Goodall

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika hafla ya upandaji miti akiwemo Esau Daudi na Faraja Zakayo wameomba wadau wa mazingira, kuendelea kutoa elimu huku wakieleza pia faida za kutunza mazingira.

Sauti ya wananchi wa kata ya bitale Kigoma

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa mwaka huu yameend sambamba na kauli mbiu isemayo Urejeshwaji wa ardhi, ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame.