Pangani FM
Pangani FM
9 October 2026, 21:39

“Zamani tulikuwa tunabwaga nazi nyingi mno kwenye minazi na pia unenepaji wa minazi na uzazi ulikuwa ni mkubwa zaidi. Lakini ongezeko hili la kina cha bahari limeathiri minazi.“
Na Cosmas Clement
Ongezeko la kina cha maji ya bahari wilayani Pangani limesababisha athari kubwa na za moja kwa moja kwenye uzalishaji na afya ya zao la minazi, ambalo ni nguzo muhimu ya kiuchumi kwa wakazi wa ukanda huo wa pwani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, nchini Tanzania linasema maji ya chumvi yamepenya umbali wa kilometa 8 ndani ya mto Pangani, hali iliyosababisha maji ya chumvi kuingia mashambani.
Kupanda kwa kina cha bahari kunafanya maji ya chumvi kuingia ndani zaidi kwenye mashamba ya minazi. Ingawa minazi hustahimili kiwango fulani cha chumvi, ongezeko kubwa la chumvi ardhini linazuia mizizi kufyonza maji safi na virutubisho. Hali hii inasababisha maisha kuwa magumu kwa wananchi waliokuwa wakitegemea zao hilo.
Je nini suluhisho?
Tafadhali fuatilia makala iliyoandaliwa na mwandishi wetu Cosmas Clement kuhusu athari na suluhu ya kupanda kwa kina cha bahari. SIKILIZA HAPA