Pangani FM

Wauguzi Pangani waombwa kuboresha mawasiliano kwa wagonjwa

12 May 2023, 1:41 pm

Na Erick Mallya

Ikiwa leo ni siku wa wauguzi duniani,wauguzi wilayani pangani mkoani tanga wameombwa kuboresha mahusiano na mawasliano baina yao na wagonjwa

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wilayani pangani walipozungumza na pangani FM katika ripoti maalum ya maadhmiho ya siku ya wauguzi mwaka 2023 kwa wilaya ya Pangani.

Sauti ya Mwananchi wa Pangani kuhusu mawasiliano ya wauguzi kwa wagonjwa Hospitali ya wilaya Pangani.

Nao wauguzi  kutoka Hospitali ya wilaya ya Pangani wamesema kuwa siku hii  itawapa nafasi ya kula kiapo cha kukumbushana wajibu na umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Sauti ya Muuguzi Mfawidhi wa Hospital ya Wilaya Pangani.

Bi Zuwena Msangi ambaye ni Muuguzi Mfawidhi wa Hospital ya Wilaya  Pangani amesema kuwa maadhimisho ya siku  hii kiwilaya yatafanyika katika hospitali hiyo leo kuanzia majira ya saa 9 Alasiri yakijumusiha shuhguli mbalimbali ikiwemo kula kiapo cha kukumbushana wajibu.