Pangani FM

Wazazi Wilayani Pangani washauriwa kuendeleza vipaji vya Watoto.

9 March 2021, 8:13 pm

Wazazi na walezi wilayani Pangani Mkoani Tanga wameshauriwa kuwaendeleza vipaji mbalimbali vya watoto wao ili kuwawezesha kufikia ndoto zao.

Hayo yameelezwa na Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Funguni RAMADHANI KAKAI wakati akizungumza na PANGANI FM

Mwalimu huyo amesema kuwa vipaji vya Watoto vinaanzia nyumbani hivyo amewataka wazazi kuwafuatilia watoto wao ili kuwasaidia kuendeleza vipaji walivyonavyo.

‘’Kwa wazazi mimi niwaombe mzazi vipaji hivi mtoto anajionyesha tangu akiwa mdogo, unaweza ukamkuta anachezea vitu na anaunda kitu tunachatakiwa ni kumuunga mkono ili aendeleze kipaji chake, kuna muda wazazi tunakosea mtoto ana kipaji hiki wewe unampeleka huku sio mbaya ila kuna muda unampoteza’’

Anesena Mwalimu Kakai

Aidha Mwalimu Kakai amesema kuwa katika kuwawezesha Wanafunzi Shuleni hapo kufikia ndoto wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kuwezesha kuendeleza vipaji vya wanafunzi hao.