Pangani FM

Miioni 80 za IMF kujenga madarasa Bushiri.

11 November 2021, 10:43 am

Viongozi wa kata ya bushiri wilayani Pangani mkoani Tanga wamepanga kuanza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa mwezi huu baada ya kupokea fedha kutoka Serikali.

Fedha hizo zinatokana na mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuinua Uchumi kwa kutumia mkopo wa fedha wa shilingi Trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF)

Pangani FM imezungumza na mtendaji wa Kata ya Bushiri Bw. Mwinyimkuu Nasoro Burhani ambaye amedai kuwa matarajio yao ni kuanza na ujenzi wa vyumba vya madarasa manne kwa kuwa tayari wameshapokea kiasi cha fedha shilingi milioni 80 na tayari Wananchi wako tayari kutoa nguvukazi yao.