Pangani FM

Jamii inawajibika vipi kupunguza hewa Ukaa

7 May 2021, 7:57 pm

Maisha ya Binadamu na viumbe wengine ulimwenguni yanategemea sana hali nzuri ya hewa safi na salama, kadhalika na mgawanyo mzuri wa hewa hizo.

Anga ya dunia inatoa mchango muhimu katika hali ya hewa ya siku husika. Iwapo tunakuwa na joto au baridi, unyevunyevu au ukavu, utulivu au dhoruba, mawingu mazito au mepesi.

Hewa hizi huamua usalama,uhai na hata ustahimilivu wa dunia dhidi ya majanga mbalimbali.

Sikiliza hapa Makala ya Nitunze nikutunze inayoangazia juu ya uwajibikaji wa jamii katika kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.