Pangani FM

Je wewe ni Mkulima? hii ni muhimu sana kwako.

23 April 2021, 8:34 pm

Dalili za wazi na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi zinazoongezeka kote duniani , huku sekta ya kilimo nayo ikionekana kuelemewa kwa kuwa   misimu ya mvua haitabiriki na nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zimekuwa zikitegemea kilimo cha mvua ..mvua ambazo zimeathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi

Taarifa za  hali ya hewa duniani zinasema majanga ya asili, ikiwemo mafuriko, vimbunga , joto la kupindukia, kuongezeka kwa kina cha baharĂ­  na matukio kama elnino vyote vinaongezeka kutokana na mabadiliko haya ya tabianchi na hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi endapo hatua madhibuti hazitochukuliwa.

Hii ni Makala ya Nitunze nikutunze msikilizaji na juma hili tunaangazia umuhimu wa wakulima kutumia taarifa za hali ya hewa ilikukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

Sikiliza hapa