Pangani FM

Madiwani wa Kata zote wilayani Pangani katika Mafunzo ya Uongozi wa ‘mguso’

7 January 2021, 5:04 pm

Madiwani wa kata 14 za wilaya ya Pangani Mkoani Tanga pamoja na viongozi wa Halmashauri (w) wameshiriki katika mafunzo ya ‘uongozi wa mguso yanayoratibiwa na shirika la UZIKWASA lililopo wilayani humo.

Mafunzo hayo yanayolenga Kumwezesha kiongozi kujimulika mwenyewe,kutafakari na katika uongozi wake na kumuongezea wito kiutendaji yanafanyika kwa siku 3 kuanzia Januari 6 hadi 8 katika Ukumbi wa Seaside uliopo wilayani Pangani.

Madiwani wa Kata mbalimbali za Pangani katika makundi ya mijadala ndani katika mafunzo hayo.

Hizi ni nukuu za baadhi ya Madiwani hao juu ya kile walichokipata kwenye mafunzo hayo kwa siku ya Kwanza.

“wakati mwingine tuvue vyeo vyetu ili tuende sawa na wanachi wetu ili kutengeneza mahusiano na mawasiliano mazuri pia kama viongozi ni vizuri kusikiliza na sio kusikia na pia unapotenga mda kwa ajili ya kumsikiliza unajenga ukaribu na wananchi wako”

Diwani Kata ya Mkwaja.

“mimi naona kama kiongozi uwe dira ya kuleta maendeleo kwa wananchi ili kufikia mafanikio wanayoyategemea wananchi wako,lakini pia kiongozi anatakiwa ajishushe na awe msikivu ili uwe mbunifu na kuruhusu vitu vipya”

Bi Salvata Kalanga ambaye ni Muezeshaji kutoka Shirika hilo amewashukuru Viongozi hao kwa kuitikia wito wa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo na pia amewasihi kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko katika Uomgozi wao na Jamii kwa ujumla.

“tumepitia michakato mikubwa na mizuri ambayo inatunoa kama viongozi na naamini kupitia warsha hii kuna vitu vingi tulivyovipata na hakuna mtu ambaye ameondoka hivihivi na amini kuna jambo jipya amelipata na litamsaidia katika safari yake ya uongozi hivyo naomba ushiriki huu uendelee katika siku nyengine ili tuzungumze kwa pamoja”

Amesema Bi. Salvata