Pangani FM

Kipumbwi yapokea Kontena la Ofisi ya Bandari.

1 January 2021, 7:52 pm

Uongozi wa Kitongoji cha Kipumbwi Mji Mpya kilichopo Kijiji cha Kipumbwi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamepokea Kontena litakalotumika kama Ofisi ya bandari hiyo.

Akithibitisha kupokea kontena hilo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Bwana JUMBE MRISHO ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Kipumbwi Mji Mpya, mbali na kutoa Shukurani zake kwa Serikali amewataka wananchi pamoja na wafanyabiashara kutumia Bandari ya Kipumbwi kwa uhuru kupitisha bidhaa zao.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. AKIDA BAHORERA ameipongeza Serikali kwa kusikia na kutatua kilio cha muda mrefu cha wakazi wa kipumbwi kwa kuirasimisha Bandari hiyo.

Diwani wa kata hiyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. AKIDA BAHORERA

Aidha Mhe. BAHORERA amesema kuwa kwasasa wanafanya taratibu za kupatikana kwa boti ya uokoaji kwa kuwa tayari bandari hiyo imesha rasimishwa, na kumekuwa na muingiliano mkubwa wa watu.