Pangani FM

Jeshi la polisi latoa ahadi kuendelea kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike

11 October 2023, 4:08 pm

ASP Majura Makemba akizungumza katika kipindi cha Asubuhi ya Leo kinachorushwa na Pangani FM.

” Siku hii inalipa nguvu Jeshi la Polisi kupaza sauti ya kukabiliana ukatili kwa mtoto wa kike”

Na Saa Zumo

Jeshi la polisi katika Wilayani Pangani Mkoani Tanga limetoa ahadi ya kuendelea kupaza sauti kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike.

Akizunguma na kituo hiki Mratibu Jeshi hilo ASP Majura Makemba amesema ili kutokomeza vitendo hivyo ni muhimu serikali kwa kushirikiana na jamii ikaendelea kuchukua hatua kwa wanaotekeleza vitendo hivyo

Sauti ya ASP Majura

Ameongeza kuwa pia elimu inapaswa kutolewa mashuleni ili kujenga uelewa kwa mtoto wa kike pindi anapoona viashairia vya vitendo vya ukatili.

Sauti ya ASP Majura

October 11 Kila mwaka Dunia uadhimisha siku ya mtoto wa kike ambapo kitaifa imefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa SPIKA wa Bunge Dokta Tulia Ackson.