Pangani FM

Serikali yachukua hatua ukosefu wa huduma za uzazi kituo cha afya Tongoni

12 August 2025, 17:49

Baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali katika kituo cha afya Tongoni Mkoani Tanga

Makala ya Afya yako ilipofika katika Kituo cha afya Tongoni mwaka 2023 ilikutana na changamoto ya kukosekana kwa huduma za uzazi. Pangani FM iliwasilisha changamoto hizo katika Serikali ya Wilaya ya Tanga, na kuahidi kwamba ingerejea tena mwaka mmoja baadae. 2025 Makala hii iliporejea tena ilikuta bado wanawake wanaotaka kujifungua kwenda katika vituo vingine vya afya lakini tayari Serikali ikiwa imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo.

Sikiliza hapa makala iliyondaliwa na Hamisi Makungu.