Pangani FM
Pangani FM
6 June 2024, 11:23

Watoto na vijana wakipata elimu ya utunzaji na uhifadhi misitu watakuwa mabalozi wazuri kuhakikisha misitu inakuwepo.
Na Hamisi Makungu
Jamii imeshauriwa kurithisha elimu ya utunzaji na uhifadhi wa misitu kwa kizazi kichanga ili kuwezesha uendelevu wa hifadhi na misitu hapa nchini.
Ushauri huo umetolewana mwalimu Gladness Masonde ambaye ni mwalimu wa mazingira katika shule ya msingi Kwezitu iliyopo tarafa ya Amani wilayani Muheza hapa mkoani Tanga.
Mh Masonde amesema wao kama shule wanarithisha elimu ya mazingira na uhifadhi kwa watoto kuanzia darasa la kwanza ili kuwajenga kuwa mabalozi wa mazingira
Mw Gladness Masonde hutoa mafunzo ya upandaji wa miti kwa vitendo anapokutana na wanafunzi wake,na hata anapoingia darasani huanza kwa kuzungumza na wanafunzi juu ya namna wanavyoendeleza somo la upandaji wa miti.
Na tukisalia katika suala la utunzaji wa mazingira wanafunzi wa shule ya msingi Boza hapa Wilayani Pangani wameeleza kutoridhishwa na vitendo vya ukataji wa miti huku wakiwashauri wazazi wao ambao wamekuwa vyanzo vya ukataji wa miti kutafuta shughuli zingine za kufanya.