Pangani FM

Wanawake Pangani waadhimisha siku ya Maombi.

5 March 2021, 10:49 pm

Wanawake wa madhehebu mbalimbali ya  Kikristo  wilayani Pangani mkoani Tanga leo wameshiriki katika  maadhimisho ya siku ya maombi ya Wanawake duniani yenye lengo la kuombea Amani na mambo mengine.

Akizungumza na PANGANI FM  mchungaji FELIX ELIASI MSUMARI wa kanisa la KKKT usharika  wa wilaya ya Pangani amesema kuwa maombi ya dunia kwa wanawake hufanyika kwa makanisa yote kwa lengo la kuwafanya walioshiriki kurudia Imani katika nafsi zao na pia  wametumia siku hiyo  kuiombea dunia dhidi ya janga la COVID 19.

leo ni siku ya maombi duniani ni siku ya maombi kwa makanisa yote duniani kwa wanawake na maombi haya yanaambatana na msingi ambao uliwekwa na nabii yeremia ambao aliomba wanawake waweze kuoomboleza kwa siku ya leo msingi mkubwa wa maombi ni kuombea dunia kwa ajili ya Amani lakini pia kuombea dunia kwa janga la COVID 19.

Amesema Mchungaji Msumari

Aidha mchungaji FELIX amewaomba wakinamama hao kutokusubiria mpaka siku ya maombi kwa ajili ya kuomba bali wawe na utaratibu wa kufanya hivyo hususani nyakati huu ambao jamii imegubikwa na vitendo vya ukatili.

“lakini natoa wito kwa wamama kwani maombi yanaendelea kila siku sio kusubiria mpaka siku ya maombi duniani ndio kuomba kwani maombi kila siku na tunawaomba wawe wanakutana kila wakati kwa ajili ya maombi hususani pia kuweza kuombea kupungua kwa vitendo vya kikatili”

Amesema Mchungaji Msumari

kwa upande wake mmoja ya Wanawake  ambao wamehudhuria katika maadhimisho hayo amesema kuwa siku hiyo kwa upande wao wanaitumia kufanya maombi hususani kuombea dhidi ya  majanga mbali mbali yanayoikumba Dunia.