Pangani FM

Mchakato wa awali ujenzi wa Soko kubwa la Samaki Kipumbwi waanza rasmi.

1 January 2021, 6:24 pm

Zoezi la utafiti wa awali kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Samaki katika kata ya Kipumbwi Wilayani Pangani Mkoani Tanga limeanza hapo jana kwa wataalam kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi kutembelea eneo linaloratajiwa kufanyika ujenzi wa mradi huo.

Akizungumza na Pangani FM wakati wa zoezi hilo Diwani wa Kata ya kipumbwi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Bwana Akida Bahorera ametoa shukrani kwa Serikali na kuelezea mtarajio yake katika mchakato huo.

Diwani wa Kaata ya Kipumbwi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Pangani. Akida Bahorera

“Nimepata faraja kwa sababu mipango hii ya Serikali inakuja katika Kata yangu kwa hiyo tumemshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu ukisoma ilani ya CCM 2020-2025 imeelezea soko la Kimataifa la Mazao ya Bahari kufanyika hapa Kipumbwi nadhani Mheshimiwa Rais anakwenda sasa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Nichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Rais na pia kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Pangani Mheshimiwa Aweso kwa kaz kubwa anayoifanya kuhakikisha anawaletea maendeleo watu wa Pangani kwa kweli fursa ya Soko hili ni Kubwa sababu litakuwa soko la Kimataifa kuna wawekezaji,wanunuzi wengi toka Nchi za Jirani watakuja kununua hapa Kipumbwi sasa inakwenda kuinuka na Wilaya nzima ya Pangani.”

Amesema Diwani wa Kata ya Kipumbwi Akida Bahorera

Kwa upande wake AFISA uvuvi mkuu kutoka makao makuu ya wizara ya mifugo na uvuvi bwana WILIAM NDAGILE amesema kuwa serikali inafahamu juu ya uhitaji wa soko katika eneo hilo.

Aidha bwana WILIAM amesema kuwa soko hilo litakuwa furusa kwa wananchi wa ndani na nje ya Pangani kupunguza kupotea kwa mazao ya Bahari napia ni sehemu ya kuongeza thamani ya mazao hayo.

Zoezi hilo limefanyika December 31 katika kata ya kipumbwi moja ya maeneo ambayo shughuli za uvuvi, usafirishaji na biashara ya Samaki vinafanyika kwa kiwango kikubwa wilayani Pangani Mkoani Tanga